Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amepokea
kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mchezaji wa zamani wa timu
ya soka ya Mtibwa Sugar ya Morogoro inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, John Mabula(Mwenye jenzi ya njano)
Mbali
ya Mtibwa Sugar, taarifa za Mabula ambaye pia amewahi kuchezea Moro
United ya Morogoro na Shinyanga Shooting ya Shinyanya kwa mafanikio
nafasi ya ulinzi kwa muda mrefu katika timu hizo, aliuawa kwa kuchomwa
kisu na mwenzake alipokuwa akiamulia ugomvi huko Kitunda - nje kidogo ya
Jiji la Dar es Salaam.
Rais
Jamal Malinzi amemwelezea Mabula kuwa ni mchezaji aliyekuwa na uwezo na
uadilifu na mchango wake katika soka utabaki katika dhana ya kumbukumbu
ya wachezaji mahiri wa Tanzania waliotokea kucheza nafasi ya ulinzi
japokuwa ametangulia mbele za haki.
Rais
Jamal Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa uongozi wa timu ambazo
alicheza ambazo ni Mtibwa Sugar, Moro United na Shinyanga Shooting;
kadhalika familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki walioguswa na
msiba huo wa gwiji huyo aliyepata pia kucheza timu ya taifa ya Vijana
wenye umri wa chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ ya mwaka 2002-2004.
Rais
Malinzi amewaasa wadau wote kuwa watulivu wakati huu mgumu wa msiba wa
mpendwa wetu Mabula hasa kutokana na mazingira ya kifo. Bwana ametoa,
Bwana Ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe. Amina.
No comments:
Post a Comment