Mhandisi
wa Miradi (TANROADS) Mkoa wa Dar es salaam Bw.Ngusa Julius akitoa
taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu ujenzi wa Barabara zinazoendelea
kujengwa ili kupunguza msongamano wa magari katika jiji La Dar es
salaam, Kulia ni Afisa Habari wa wakala huo Bi Aisha Malima.
Frank Mvungi-Maelezo.
SERIKALI
yatumia Bilioni 2 kulipa Fidia ili kusaidia kukamilisha mradi wa ujenzi
wa Barabara kwa kiwango cha lami kati ya Tanki Bovu na Goba Jijini Dar
es salaam.
Kauli
hiyo imetolewa na Mhandisi wa Miradi wa TANROADS Mkoa wa Dar es salaam
Bw. Ngusa Julius wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar
es salaam.
Akifafanua
Mhandisi Ngusa amesema kuwa fidia kwa wakazi hao itakamilika kulipwa
wiki hii ili kazi ya ujenzi wa Barabara hiyo iweze kukamilishwa kwa
wakati hali itakayosaidia kupunguza msongamano wa magari.
“Ujenzi
wa barabara hii ukikamilika utasaidia kwa Kiasi kikubwa kupunguza
foleni kwa kuwa itakuwa kiungo kati ya wakazi wa Mbezi Beach na Kimara
na maeneo mengine ya jiji la Dar es salaam.” Alisisitiza Mhandisi Ngusa.
Kwa
upande wa Barabara ya kinyerezi Kifuru Mhandisi Ngusa amesema kuwa
Milioni 431 zimetumika kulipa fidia na ujenzi wa Barabara hiyo
unaendelea.
Miradi
ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lamai inayotarajiwa kukamilika
katika kipindi hiki cha mwaka wa fedha 2015/2016 itasaidia kupunguza
msongamano wa magari kwa kiwango kikubwa katika jiji la Dar es salaam.
Awamu
ya Tatu ya ujenzi itahusisha barabara za Goba - Wazo hill -Tegeta
Kibaoni (13.0Km), Mbezi Mwisho - Malambamawili- Kifuru (6kM), Goba -
Makongo ardhi (9km ) na Pia kukamilisha usanifu wa outering road Bunju B
- Mpiji Magohe - Victoria Kifuru hadi Pugu kiltex 33.7.
Wakala
wa Barabara nchini TANROADS unatekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa
barabara katika jiji la Dar es salaam kwa kiwango cha lami ambapo
barabara hizo zinatarajiwa kuondoa tatizo la msongamano wa magari katika
jiji hilo.
No comments:
Post a Comment