Polisi wanashuku kuwa mashindano hayo yanayokiuka sheria za barabarani mbali na kuhatarisha maisha ya waendeshaji wengine wa magari huwa yanaandaliwa na matajiri wanaomiliki magari ya kifahari.
Aid polisi wanashuku matajiri hao huweka dau kisha kuwaajiri madereva kushindana mabarabarani.
Polisi walikuwa na wakati mgumu kuwakamata washukiwa kwani waliendesha magari yao kwa kasi zaidi ya kilomita 290 kwa saa.
Polisi walimudu tu kuwatia mbaroni baada yao pia kuyatumia magari ya kifahari yanayomilikiwa na polisi.
Washukiwa watatozwa faini ya dola 27,000 kila mmoja. Wamiliki wa magari hayo wanatakriban siku 90 kulipa ada ya dola elfu 13,500 la sivyo magari yao yapigwe mnada.
Utafiti unaonesha kuwa mabwenyenye Dubai ndio wanaomiliki magari mengi zaidi ya miji mikuu ya London na hata New York.
No comments:
Post a Comment