MSHAMBULIAJI Lukas Podolski ameihama Arsenal na
kujiunga na Galatasaray, kwa mujibu wa mabingwa hao wa Uturuki na jana
alitarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya yake kukamilisha uhamisho huo.
Mjerumani
huyo mwenye umri wa miaka 30, alijiunga na Arsenal akitokea FC Koln ya kwao
mwaka 2012 kwa ada ya pauni milioni 11 na alifunga mabao 31 katika mechi 82 kwa
klabu hiyo ya London.
Podolski aliisaidia kubeba Kombe la FA mwaka 2013, lakini alitumia
sehemu ya pili ya msimu uliopita akiwa kwa mkopo Inter Milan.
No comments:
Post a Comment