MAKADA 231 wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
mkoani Rukwa wamerejesha fomu za kuwania nafasi
za ubunge na udiwani kupitia chama
hicho katika Uchaguzi
Mkuu ujao.
Katibu wa Chadema Mkoa
wa Rukwa, Ozem Chapita, alibainisha
kuwa uchukuaji wa fomu ulianza
Mei 18 na kumalizika Juni 25, mwaka huu.
Alisema
kukua kwa demokrasia kumeongeza idadi ya makada wa chama hicho waliojitokeza kuchukua
fomu na kuzirejesha kwa wakati
katika majimbo yote matano
yaliyopo mkoani humo.
Alibainisha kwa nafasi
ya ubunge katika majimbo hayo
matano, makada 29
walijitokeza kuchukua na kurejesha
fomu wakiwemo watano
wa viti maalumu.
“Makada wa chama chetu wanaowania
nafasi ya udiwani ni 143 viti
maalumu wakiwa 54
hii ni kwa mkoa mzima,” alisisitiza.
No comments:
Post a Comment