KOCHA wa klabu ya Bayern Munich,
Pep Guardiola amesisitiza kuwa,
klabu hiyo haina mpango wa kumsajili mchezaji Angel
Di Maria wa Manchester United kwenye msimu huu wa usajili.
Pia aliongeza kuwa fedha zinazotumika kwa ajili ya usajili wa wachezaji
wakubwa ni nyingi ambazo hazistahimiliki.
Mchezaji huyo ni moja kati ya wachezaji ambao wamesajiliwa kwa kiasi
kikubwa cha fedha, ambapo alipochukuliwa na Manchester United akitokea Real
Madrid alichukuliwa kwa kitita cha pauni Milioni 59.7.
Lakini hata hivyo anakabiliwa na changamoto ya kushindwa kucheza
kulingana na kitita hicho cha fedha alichonunuliwa.
Kutokana na hali hiyo kumekuwa na tetesi kuwa kuna uwezekano wa klabu
hiyo ya Manchester United kuachana na mchezaji huyo na watu wamekuwa wakihisi
kuwa huenda angechukuliwa na Guadiola.
Guardiola alisema kuwa kwa upande wake hana haja ya kumchukua mchezaji
huyo kwa kuwa tayari kwenye kikosi chake kuna wachezaji wakubwa na wenye uwezo
zaidi.
Alisema kuwa tayari imemchukua mchezaji Douglas Costa kutoka Brazil na
hawana haja tena ya kuongeza mchezaji mwengine kwa sasa.
Alisema kuwa hana haja ya kumchukua mchezaji huyo kwa kuwa kwanza anajua uwezo wake wa uchezaji na kiwango chake pia na kwa sasa anamuona ni kama mchezaji ambae ni msaada mkubwa kwa timu yake aliyopo ya Manchester United.
"Sioni kama klabu yake hiyo ilifanya kosa kumchukua ila ilikuwa
ikijua inachokifanya na uwezo wake ni mkubwa tu hivyo wacha aendelee kutumikia
huko."
No comments:
Post a Comment