Saturday, June 20, 2015

ZIARA ya WAANDISHI WA HABARI TANZANIA KWENYE VIVUTIO VYA UTALII ZIMBABWE



IMG_2873
Mungoza watalii katika mapango ya Chinhoyi katika mkoa wa Chinhoyi nchini Zimbabwe, Aleck Makumire akitoa maelezo wa timu ya waandishi wa habari kabla ya kushuka kwenye mapango hayo wakati wa ziara maalum ya kutembelea vivutio vya Utalii nchini humo.
 *************
Na Modewjiblog team, Harare
Waandishi wa habari kutoka vyombo 5 vya habari vya magazeti ya Tanzania ikiwemo mtandao wa habari wa modewjiblog ambao ni Justin Damiana (The African), Frank Aman (The Guardian), Zainul Mzige (modewjiblog), Mariam Said (Daily News) pamoja na Timothy Kitundu (East Africa Business Week) walipata mwaliko kutoka Mamlaka ya Utalii ya Zimbabwe (ZTA) kufanya utalii katika mapango ya Chinhoyi, Ziwa Kariba, Shamba la ufagaji wa Mamba, Hifadhi ya Taifa ya Kariba, Bandari ya Zambezi pamoja na ukuta wa bwawa la Kariba unaotengenisha nchi ya Zambia na Zimbabwe.
Safari ya kuelekea nchini Zimbabwe ilidhaminiwa na Shirika la usafiri wa Anga wenye gharama nafuu Fastjet Tanzania ikiwa ni moja ya mipango yao ya kuimarisha safari zake za kutoka Dar es Salaam-Lusaka na Harare.
Safari hiyo ilikuwa maalum kwa ajili kuhudhuria maonyesho ya naneya Kimataifa ya Utalii Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) ambayo yameanza kurindima jijini Harare katika ukumbi wa Harare International Conference Centre (HICC).
 IMG_2896
Mungoza watalii katika mapango ya Chinhoyi katika mkoa wa Chinhoyi nchini Zimbabwe, Aleck Makumire akiwa ndani ya mapango ya Chinhoyi akitoa maelezo kwa waandishi wa habari wa Tanzania katika ziara yao ya kutembelea vivutio vya utalii nchini humo.
IMG_2921
Waandishi wa habari kutoka Tanzania waliosafirishwa na Shirika la ndege lenye gharama nafuu nchini Fastjet kuhudhuria maonyesho ya Kimataifa ya Utalii ya Shanganai yanayoendelea nchini Zimbabwe. Kutoka kushoto ni Timothy Kitundu (East Africa Business Week), Mariam Said (Daily News) pamoja na Justin Damiana (The African) wakiwa wameketi kwenye mapango ya Chinhoyi huku wakibadilishana mawazo na wadau wa utalii kutoka Afrika Kusini.
IMG_2943
Mwandishi wa habari Timothy Kitundu (East Africa Business Week) akitoka kudhuru mapango hayo wakati wa ziara ya kutembelea vivutio vya utalii.
IMG_2956
Picha ya pamoja na wenyeji wetu....
PICHA ZAIDI FATHER KIDEVU BLOG

No comments:

Post a Comment