
Klabu ya Simba leo imetangaza kuingia mkataba wa mwaka mmoja na Dylan Kerr kama kocha mpya anayechukua mikoba ya Goran Kopunovic na anatarajiwa kuanza kazi rasmi mwanzoni mwa mwezi July.
Akimtangaza kocha huyo,Raisi wa klabu ya
Simba Evans Aveva amesema kuwa Kocha huyo kutoka Nchini Uingereza ana
uzoefu wa zaidi ya miaka 30 katika fani ya mpira wa miguu huku pia akiwa
na umahiri wa kufundisha klabu mbalimbali duniani zikiwemo Hai Phong FC
Vietnam, Hamilliton Academicals FC na Greennock Morton FC zote kutoka
Scotland.
Kocha Kerr pia ana uzoefu wa kufundisha
na kufanya kazi Afrika, ameshawahi kufanya kazi na kufundisha timu za
South Africa NFD Nathi Lions FC na South Africa Thanda Royal Zulu FC
kutoka Afrika Kusini....
Aveva ameongeza kuwa Klabu ya Simba
inafuraha kubwa kuingia mkataba na kocha huyu mwenye uzoefu na weledi wa
kutosha, na wana amini atakuwa chachu ya mafanikio pia kwa kunoa vipaji
vya wachezaji wa Simba.
Kerr ana leseni ya daraja A na B ya
ukocha aliyotunukiwa na Shirikisho la soka la Ulaya (UEFA) huku pia
akiwa na uzoefu wa utawala katika fani ya michezo.
Kwa taarifa zaidi za wasifu wa Kocha Dylan Kerr ...BONYEZA HAPA
No comments:
Post a Comment