KOCHA MPYA WA SIMBA HUYU HAPA - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA


Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, June 22, 2015

KOCHA MPYA WA SIMBA HUYU HAPA

Klabu ya Simba leo imetangaza kuingia mkataba wa mwaka mmoja na Dylan Kerr kama kocha mpya anayechukua mikoba ya Goran Kopunovic na anatarajiwa kuanza kazi rasmi mwanzoni mwa mwezi July.

Akimtangaza kocha huyo,Raisi wa klabu ya Simba Evans Aveva amesema kuwa Kocha huyo kutoka Nchini Uingereza ana uzoefu wa zaidi ya miaka 30 katika fani ya mpira wa miguu huku pia akiwa na umahiri wa kufundisha klabu mbalimbali duniani zikiwemo Hai Phong FC Vietnam, Hamilliton Academicals FC na Greennock Morton FC zote kutoka Scotland.

Kocha Kerr pia ana uzoefu wa kufundisha na kufanya kazi Afrika, ameshawahi kufanya kazi na kufundisha timu za South Africa NFD Nathi Lions FC na  South Africa Thanda Royal Zulu FC kutoka Afrika Kusini....

Aveva ameongeza kuwa Klabu ya Simba inafuraha kubwa kuingia mkataba na kocha huyu mwenye uzoefu na weledi wa kutosha, na wana amini atakuwa chachu ya mafanikio pia kwa kunoa vipaji vya wachezaji wa Simba.

Kerr ana leseni ya daraja A na B ya ukocha aliyotunukiwa na Shirikisho la soka la Ulaya (UEFA) huku pia akiwa na uzoefu wa utawala katika fani ya michezo.

Kwa taarifa zaidi za wasifu wa Kocha Dylan Kerr ...BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here