
RADAMEL Falcao amebainisha kuwa uhamisho wa mkopo
kwenda kwa mabingwa wa Ligi Kuu ya England, Chelsea utakamilishwa katika siku
chache zijazo.
Mshambuliaji
huyo wa Colombia amekuwa akihusishwa na uhamisho wa mkopo wa muda mrefu kwa
Chelsea ambayo kocha wake Jose Mourinho ametangaza kuwa atamnyakua kwa mkopo
Falcao.
Mshambuliaji
huyo wa zamani wa Atletico Madrid aliichezea Manchester United kwa mkopo msimu
uliopita akitokea Monaco.
Hata
hivyo, baada ya msimu ambao alifunga mabao manne tu katika mechi 29 kwa
mashindano yote, United iliamua kutotumia fursa waliyopewa ya kumsajili kwa
mkataba wa kudumu.
Hata
hivyo, Chelsea inaonekana kujiandaa kumpa nafasi Falcao ambaye aliwaambia
waandishi wa habari: “Ninawaza Copa America na kikosi chetu, wafanyakazi wangu
wanashughulikia hilo (la uhamisho).”
Alipoulizwa
kama ripoti za uhamisho wa mkopo kwenda Chelsea ni sahihi, Falcao akizungumza
baada ya ushindi wa bao 1-0 wa Colombia dhidi ya Brazil, aliongeza:
“Inawezekana, mtafahamu hivi karibuni.”
No comments:
Post a Comment