BARCELONA YAFIKIRIA HISTORIA ZAIDI - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA


Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, June 9, 2015

BARCELONA YAFIKIRIA HISTORIA ZAIDI



FC BarcelonaLUIS Enrique anasema kuwa Barcelona sasa ina lengo la kuwa klabu ya kwanza kutetea taji la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya wakati kocha wake mkuu akifikiria hatma yake licha ya kuweka historia ya kutwaa mataji matatu kwa mara moja.

Luis Suarez na Neymar walifunga mabao katika kipindi cha pili na kuiwezesha Barcelon akuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Juventus Jumamosi wakati timu hiyo ya Hispania ikiwa ya kwanza kushinda mara mbili taji la Ulaya.

Enrique alikuwa akiifundisha Barcelona katika msimu wake wa kwanza kama Kocha Mkuu baada ya Pep Guardiola kuiwezesha timu hiyo kutwaa taji la Ulaya, Hispania na lile la Ligi katika msimu wa mwaka 2008/09.

Bao la mapema lililowekwa kimiani na Ivan Rakitic lilifutwa na lle la Juventus lililofungwa na mchezaji wazamani wa Real Madrid Alvaro Morata alisawazisha katika dakika ya 55.

Lakini Suarez aliwafanya washindi kuwa mbele baada ya kuwafungia bao la pili katika dakika ya 68 katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Olimpiki jijini Berlin kabla Neymar hajaongeza la tatu katika dakika ya 97.

Kwa ushindi huo, Barcelona sasa imeshinda mara tano taji hilo la Ulaya baada ya kushinda mwaka 1992, 2006, 2009 na 2011.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here