ASTON VILLA YAMTAKA KAKA WA POGBA - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA


Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, June 8, 2015

ASTON VILLA YAMTAKA KAKA WA POGBA





KLABU ya Aston Villa inamuwania beki wa kati wa Saint Etienne, Florentin Pogba, L’Equipe limeripoti.
Kukiwa na tetesi juu ya hatima ya beki tegemeo Ron Vlaar, the Villans ipo sokoni kusaka mbadala wake.
L’Equipe limesema kwamba mchezaji wa Saint Etienne Florentin Pogba ametajwa kuwa miongoni mwa wanaowaniwa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye ni kaka wa Paul anayecheza Juventus, amekuwa na msimu mzuri.
Mkataba wake ukiwa umekwisha zaidi ya mwaka mmoja, Saint Etienne haina chaguo zaidi ya kumuuza hasa ikizingatiwa kuwa mchezaji huyo alikataa kuongeza mkataba.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Guinea amecheza mechi 16 pekee msimu huu, akikosa namba ya kudumu kwenye kikosi kutokana na kusumbuliwa na majeraha

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here