AGUERO, Di MARIA WAIUA BOLIVIA - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA


Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, June 8, 2015

AGUERO, Di MARIA WAIUA BOLIVIA

 
SERGIO Aguero amefunga ‘hat-trick’ ya kwanza kwenye timu ya taifa wakati Argentina ilipoifunga Bolivia mabao  5-0 katika mechi ya kirafiki kujiandaa na michuano ya Copa America, inayotarajiwa kuanza Alhamisi ya wiki hii. 
 
Winga wa Manchester United Angel Di Maria alifunga bao la kuongoza kwa timu yake katika dakika ya 24. 

Mshambuliaji wa Manchester City Aguero aliongeza bao la pili kwa mkwaju wa penalti na kisha kufunga la tatu kwa kuunganisha mpira wa kona.

Aguero alikamilisha ‘hat-trick’ yake kwa kufunga bao la nne na Di Maria akafunga bao lake la pili na kuhitimisha karamu hiyo ya mabao matano.

Michuano ya Copa America inatarajiwa kufanyika Chile huku Argentina ikijaribu kushinda taji kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1993.

Argentina ipo kwenye kundi linalojumuisha mabingwa watetezi Uruguay, Paraguay na Jamaica.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here