VIDEO: MRISHO MPOTO, DAYNA NYANGE & AFANDE SELE - MKUHUMI, WIMBO MAALUMU WA KUHAMASISHA UTUNZAJI MAZINGIRA - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA


Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, June 9, 2015

VIDEO: MRISHO MPOTO, DAYNA NYANGE & AFANDE SELE - MKUHUMI, WIMBO MAALUMU WA KUHAMASISHA UTUNZAJI MAZINGIRA


WIMBO wa kuhamasisha utunzaji wa mazingira  wa ‘Mkuhumi’ umezinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam, huku ukitarajiwa kuleta mabadiliko miongoni mwa wananchi.
Wimbo huo ulioimbwa na wanamuziki wa kizazi kipya Seleman Msindi ‘Afande Sele’, Dayna Nyange pamoja na mwanamuziki wa kughani mashairi, Mrisho Mpoto maarufu kama ‘Mjomba’.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa wimbo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu nchini (Mjumita), Rahima Njaidi alisema, wameamua kuwatumia wasanii hao kwa kuwa ni rahisi kufikisha ujumbe kwa jamii.
Alisema lengo kuu la wimbo huo ni kuwahamasisha wananchi kutunza mazingira ili waweze kunufaika na Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kutokana na ukataji na uharibifu wa Misitu (Mkuhumi), kupitia fedha zinazotolewa na nchi zenye viwanda...
“Watu wengi tunapoenda kusikiliza muziki kuliko kusoma, kwa maana hiyo kama tungeweka elimu hii kwenye vipeperushi isingekuwa rahisi kwa watu wote kupata ujumbe, lakini tunategemea kupitia muziki huu tutawafgikia watu wengi,” alisema.
Alisema wimbo huo umetayarishwa chini ya usimamizi wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Mkuhumi ili kuwafikia wadau ili kwa pamoja waweze kuchukua tahadhari na kupunguza shughuli zinazochangia kutokea kwa mabadiliko ya tabia nchi.
“Kupitia wimbo huu jamii itapata uelewa utakaosaidia kuhamasisha jamiikutumia rasilimali za misitu kwa njia ya uendelevu na kujipatia faida,” alisema Njaidi.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here