KLABU ya Aston Villa inamuwania beki wa kati wa Saint
Etienne, Florentin Pogba, L’Equipe limeripoti.
Kukiwa
na tetesi juu ya hatima ya beki tegemeo Ron Vlaar, the Villans ipo sokoni kusaka
mbadala wake.
L’Equipe
limesema kwamba mchezaji wa Saint Etienne Florentin Pogba ametajwa kuwa
miongoni mwa wanaowaniwa.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye ni kaka wa Paul anayecheza Juventus,
amekuwa na msimu mzuri.
Mkataba
wake ukiwa umekwisha zaidi ya mwaka mmoja, Saint Etienne haina chaguo zaidi ya
kumuuza hasa ikizingatiwa kuwa mchezaji huyo alikataa kuongeza mkataba.
Mchezaji
huyo wa kimataifa wa Guinea amecheza mechi 16 pekee msimu huu, akikosa namba ya
kudumu kwenye kikosi kutokana na kusumbuliwa na majeraha

No comments:
Post a Comment