SERGIO Aguero amefunga ‘hat-trick’ ya kwanza kwenye
timu ya taifa wakati Argentina ilipoifunga Bolivia mabao 5-0 katika mechi ya kirafiki kujiandaa na
michuano ya Copa America, inayotarajiwa kuanza Alhamisi ya wiki hii.
Winga
wa Manchester United Angel Di Maria alifunga bao la kuongoza kwa timu yake
katika dakika ya 24.
Mshambuliaji
wa Manchester City Aguero aliongeza bao la pili kwa mkwaju wa penalti na kisha
kufunga la tatu kwa kuunganisha mpira wa kona.
Aguero
alikamilisha ‘hat-trick’ yake kwa kufunga bao la nne na Di Maria akafunga bao
lake la pili na kuhitimisha karamu hiyo ya mabao matano.
Argentina
ipo kwenye kundi linalojumuisha mabingwa watetezi Uruguay, Paraguay na Jamaica.
Michuano
ya Copa America inatarajiwa kufanyika Chile huku Argentina ikijaribu kushinda
taji kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1993.
No comments:
Post a Comment