18 KUSHIRIKI MAMA SHUJAA WA CHAKULA - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA


Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, June 8, 2015

18 KUSHIRIKI MAMA SHUJAA WA CHAKULA



Jopo la Majaji, Kutoka Kulia ni Zephaniah Muggitu wa Digital Consulting Ltd, Jairos Mahenge Mhifadhi Mwandamizi wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu, Dora Myinga Mkulima na Mjasiliamali, Mwandiwe Makame Mkulima na Mfugaji, Roselyn Kaihula kutoka Ekama Development
WANAWAKE 18 kutoka mikoa 21 nchini, wameteuliwa kushiriki shindano la Mama Shujaa wa Chakula kwa mwaka 2015/2016, baada ya mchakato wa usahihishaji wa fomu uliofanyika kwa muda wa wiki moja.

Akizungumza Dar es Salaam jana katika hafla ya kuwatangaza washindi hao, Meneja Utetezi na Ushawishi wa Oxfam Tanzania, Eluka Kinondoni alisema fomu 26,500 zilisambazwa nchini kwa ajili ya usaili, na wanawake mbalimbali walizitumia kujaza madodoso yaliyoainishwa.

Alisema, kuna mchakato mwingine wa tatu wa kuwatafuta 15 bora watakaoingia kijijini na kuwatembelea akinamama katika maeneo wanamoishi kuhakiki waliyoyajaza.

Kwa upande wake, Mtaalamu wa Miradi ya Maendeleo kutoka Kampuni ya Diligent Consulting Limited, Zephaniah Mugittu alisema, mchakato wa kuwapata washiriki wa mwaka huu, ulikuwa mgumu kutokana na kushirikisha mikoa mingi  bara na visiwani.

“Utaratibu tulioutumia kupata washiriki, ulizingatia sekta tatu; kilimo, ufugaji na uvuvi. Kilichofuata ilikuwa ni kuwapata walioshinda zaidi ya alama 50, tukafanikiwa kupata watu wengi.

"Lakini tukasema lazima tuhakiki kwa mara ya nne na kupata majina 21. Tulihakiki tena kwa kigezo cha umri na mengineyo na kufanikiwa kuwapata 18 bora,” Mugittu alisema.

Naye Roselyn Kaihula kutoka Ekama Development Foundation alisema, fomu zilizosambazwa kwa mwaka huu ni 26,500 na zilizorudi kwa ajili ya kuhakikiwa ni 2317, ambazo zilisahihishwa na nyingine zilikuwa zimeharibika kutokana na kujazwa tofauti.

Mhifadhi Mwandamizi wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu, Jairos Mahenge alisema, shindano hilo kwa upande wa serikali linatambulika kwani linakuza kilimo na kutoa mchango mkubwa kwa sekta hiyo nchini.

Wakati huohuo Mama Shujaa wa Chakula 2011 Mwandiwe Makamekali kutoka Kaskazini Unguja, alisema majina hayo yamepatikana bila upendeleo na imeonesha kwamba wanawake wanazidi kujituma kila mwaka ili wapate nafasi hiyo, hivyo linakuza uchumi na kuwapa moyo kinamama.

Majina yaliyoingia katika mchakato wa awali ni pamoja na Getrude Mngala (Mwanza), Winnie Malya (Kilimanjaro), Dinna Samweli Sumari (Arusha), Tatu Ramadhani Kiluwa (Lushoto), Edina Gabriel Kiogwe (Dar es Salaam), Neema Kilonga (Manyara), Pili Kashinde (Itamba Kaskazini), Eva Mgeni Daudi (Pwani), Hawa Athman Mkata (Mtwara).

 Wengine ni Wanduta Daudi Kitowelo (Singida), Shida Daudi Mwedugo (Dodoma), Hellen Materu (Iringa), Upendo Paulos Mhomisoli (Njombe), Savera Mtarihabwa (Bukoba), Caroline Chelele (Morogoro), Stela Masulya (Mwanza), Regina Kampili Stephano (Katavi), Rehema Daniel Ukali (Rukwa).

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here