LUIS
Enrique anasema kuwa Barcelona sasa ina lengo la kuwa klabu ya kwanza kutetea
taji la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya wakati kocha wake mkuu akifikiria hatma yake
licha ya kuweka historia ya kutwaa mataji matatu kwa mara moja.
Luis
Suarez na Neymar walifunga mabao katika kipindi cha pili na kuiwezesha Barcelon
akuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Juventus Jumamosi wakati timu hiyo ya
Hispania ikiwa ya kwanza kushinda mara mbili taji la Ulaya.
Enrique
alikuwa akiifundisha Barcelona katika msimu wake wa kwanza kama Kocha Mkuu
baada ya Pep Guardiola kuiwezesha timu hiyo kutwaa taji la Ulaya, Hispania na
lile la Ligi katika msimu wa mwaka 2008/09.
Bao
la mapema lililowekwa kimiani na Ivan Rakitic lilifutwa na lle la Juventus
lililofungwa na mchezaji wazamani wa Real Madrid Alvaro Morata alisawazisha
katika dakika ya 55.
Lakini
Suarez aliwafanya washindi kuwa mbele baada ya kuwafungia bao la pili katika
dakika ya 68 katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Olimpiki jijini
Berlin kabla Neymar hajaongeza la tatu katika dakika ya 97.
Kwa
ushindi huo, Barcelona sasa imeshinda mara tano taji hilo la Ulaya baada ya
kushinda mwaka 1992, 2006, 2009 na 2011.
No comments:
Post a Comment