Bondia Baina Mazora
Baina Mazora katika moja ya mapambano yake
Bondia Francis Miyeyusho
BONDIA anayekuja kwa kasi katika masumbwi Baina Mazola(Simba wa Mazola) amejigamba kuibuka na ushindi dhidi ya bondia mkongwe Francis Miyeyusho katika pambano lao linalotarajiea kufanyika Agosti 26 mwaka huu katika ukumbi wa vijana Kinondoni.
Akizungumza na gazeti hili kwa kujigamba, Mazola alisema kuwa amejiweka vizuri kutokana na mazoezi makali anayoyafanya hivyo hana shaka yoyote kuwa "atamkalisha" Miyeyusho.
"Unajua kila kitu mazoezi, nami siyo mvivu katika hilo, imani yangu nitaibuka na ushindi siku hiyo kikubwa naomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuja kushuhudia pambano" alisema Mazola
Alisema anamheshimu sana Miyeyusho isipokuwa kwenye mchezo ni lazima mshindi apatikane hivyo nji yeye ambaye mwisho wa siku ataibuka na ushindi huo kutokana na umri wake pamoja na uwezo alinao.
Mazola alisema pamoja ba umaarufu alionao Miyeyusho yeye haoni kama ni tatizo hata yeye ataupata umaharufu huo baada ya pambano hilo la uzito wa unyoa (fly weight) kilo 57 lililoandaliwa na kampuni ya Dragon Boxing Promotion.
Hata hivyo alisema malengo yake kwa sasa ni kuhakikisha anajitengenezea jina kimataifa na kwamba ushindi katika mchezo huo ujao ndiyo utazidi kumsafishia njia katika safari yake hiyo ya kutambulika kimataifa.
Mazola alisema mchezo wa mashumbwi ni miongoni mwa michezo inayoweza kumpaisha kimataifa bondia yoyote mwenye malengo hivyo nia yake ni kutimiza ndoto za siku nyingi alizojiwekea katika masumbwi.
Aidha amewaomba wadau wapenda mchezo wa masumbwi kuendelea kuuthamini mchezo huo kwa lengo la kuitangaza Tanzania nje.
No comments:
Post a Comment