BENKI ya
Wananchi wa Tandahimba (TACOBA) mkoani Mtwara imeendelea na mikakati yake ya
kujiimarisha kwa kuuza hisa zake ikiwa ni lengo la kuongeza mtaji.
Akizungumza
na wananchi wakati wa harambee ya ununuzi wa hisa za benki hiyo iliyofanyika
Tandahimba, Meneja Mkuu Benki ya Tacoba, Mgwagi Stephen amsema mipango
yote ya kuifanya benki hiyo iwe shindani katika huduma za kibenki nchini
imekamilika.
Stephen
ameitaja baadhi ya mikakati hiyo kuwa ni kuhakikisha benki inauza hisa zake
ndani na nje ya Tandahimba kwa lengo la kuifanya iwe benki ya watu wa kusini.
Katika
harambee hiyo iliyokusanya ahadi ya Sh milioni 752, amesema zipo changamoto
nyingi zilizojitokeza tangu imeanzishwa, lakini uzoefu umewaonesha kwamba
hakuna lisilowezekana. Aliwataka wananchi wote kuchangamkia hisa hizo
zinazouzwa Sh 1,000 kila moja.
No comments:
Post a Comment