TIGO, RITA, UNICEF NA GSMA WASHIRIKIANA KUSAJILI VYETI VYA WATOTO NCHINI - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA


Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, July 14, 2017

TIGO, RITA, UNICEF NA GSMA WASHIRIKIANA KUSAJILI VYETI VYA WATOTO NCHINI

 Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Kampuni ya Millicom, Mohamed Dabour (katikati), akimkabidhi cheti cha kuzaliwa mmoja wa akina mama aliyempeleka mtoto wake kumsajili katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke Dar es Salaam leo. Mpango huo unasimamiwa na Kamuni ya simu za mkononi ya Tigo, Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA),Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto ( UNICEF) na GSMA. Kutoka kulia waliosimama ni Mtaalamu wa Masuala ya Watoto kutoka Unicef, Bhashar Mishra na Makamu wa Rais wa Mambo ya Nje wa Kampuni ya Millicom, Rachel Samren. 

 Mtaalamu wa Masuala ya Watoto kutoka UNICEF, Bhashar Mishra (kulia) akiteta jambo na maofisa waliopo katika mpango huo. Kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael.
 Ofisa Mwandamizi wa Rita, Beatrice Mboya (kulia), akielekeza jinsi vyeti vya watoto vinavyosajiliwa kwa njia ya mtandao.
Meneja Huduma za Jamii wa Tigo, Halima Okash akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tigo ilivyodhamini mpango huo.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Tigo kwa kushirikiana na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA),Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto ( UNICEF) na GSMA wametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke jijini Dar es Salaam kuona zoezi la usajili wa watoto walio chini ya miaka mitano jinsi wanavyopata vyeti vya kuzaliwa kupitia mpango maalumu unaosimamiwa na taasisi hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo,  Meneja wa masuala ya kijamii wa Tigo, Halima Okash alisema Tigo kama mdhamini wa mpango huo wa upatikanaji kwa urahisi wa vyeti hivyo kwa njia ya mtandao , kama kampuni ya mawasiliano wameamua kushirikiana na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) bega kwa bega kuhakikisha watoto wanapata vyeti vyao kwa urahisi na hadi sasa zaidi ya watoto milioni 1.6 wamepata vyeti kwenye mikoa saba nchini. 

Kwa upande wake Meneja Masoko na  Mawasiliano wa Rita,  Josephat Kimaro amesema kwa sasa wamesaji watoto mikoa saba na kuwa wamejipanga kuendelea mikoa ya kusini ambapo amewataka wazazi wajitokeze kupata vyeti vya kuzaliwa vya watoto wao. 

Alitaja mikoa waliyokwisha fanya usajili huo kuwa ni Shinyanga, Mbeya , Njombe, Mwanza, Iringa, Geita na Temeke.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here