Aliyekuwa Mstahiki Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob |
Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob jana aliwaaga madiwani wa halmashauri hiyo huku akisema Ukawa imejipanga kunyakua viti vya umeya na naibu wake wa manispaa zaKinondoni na Ubungo, huku wakiwa na idadi ya madiwani wengi.
Ahadi hiyo ya Jacob imeibua vita mpya ya kinyang’anyiro baada ya CCM nayo kutamba kwamba itaibuka kidedea katika halmashauri hizo.
Jacob alieleza jana kwamba kwa idadi kubwa wajumbe wa Ukawa ilionao, umoja huo utaibuka kidedea na kusema itashangaza kama CCM inajipa matumaini ya kushinda wakati idadi ya wajumbe wake ni ndogo.
Akizungumza katika mkutano huo Jacob mbali ya kuwashukuru wafanyakazi na wananchi wa Manispaa ya Kinondoni kwa ushirikiano waliompa katika kipindi cha miezi saba(7) aliyodumu kama Meya alitoa mchanganuo wa Madiwani wa Manispaa za Ubungo na Kinondoni baada ya kugawanywa jinsi zitakavyokuwa kama alivyochanganua hapa..
SOMA HAPA
A. HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO.
Katika Manispaa ya Ubungo Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kina viti vya Madiwani 10 na Idadi ya wabunge wa Majimbo(Ubungo na Kibamba) 2, Chama Cha Wananchi(CUF) kina viti vya Madiwani 2, na Chama Cha Mapinduzi(CCM) kina viti vya Madiwani 2 na Madiwani wa Viti Maalum 2.
Ukiachilia mbali CCM,CHADEMA na CUF katika Halmashauri ya Ubungo havina Madiwani wa viti Maalumu. Kwa hesabu hizo hapo juu katika Halmashauri ya Manispàa ya Ubungo ,CHADEMA inajumla ya Madiwani 10 na wabunge 2 hivyo Jumla kuwa 12, na CUF Madiwani 2,
hivyo kufanya UKAWA kuwa na idadi ya Madiwani 14.Na CCM kuwa na Jumla ya Madiwani 4.
Hivyo ni wazi kwamba UKAWA wataongoza Manispaa ya Ubungo.
B. HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI.
Katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kina viti vya Madiwani 8(kawe 5 na Kinondoni 3), wabunge wa Jimbo 1(kawe),Madiwani wa viti maalum 7,na Chama Cha Wananchi(CUF) kina viti 3,Madiwani Viti Maalum 2 na Mbunge wa Jimbo 1(kinondoni) na Chama Cha Mapinduzi(CCM) kina viti 9(kawe 5 na Kinondoni 4),Madiwani wa viti maalum 2 wateule wa Rais 3 na wabunge wa vitu maalum 2.
Kwa hiyo CHADEMA ina viti vya Madiwani 17 na CUF ina viti 7 na CCM ina viti 16, hivyo haihitaji miujiza kujua kuwa kwamba Halmashauri ya Kinondoni itaongozwa na UKAWA. Hii itakuwa na maana
UKAWA 24
CCM 16
No comments:
Post a Comment