TAARIFA KWA UMMA
MHESHIMIWA RAIS AJIONDOE KWENYE HILI LA KUHUJUMU MAMEYA WA UPINZANI.
Ndugu wananchi na wakazi wa *Manispaa ya Kinondoni*, nianze kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuepushia mabalaa na kutujalia Afya njema.Hatuna la kumlipa zaidi ya kusema ahsante.
Leo
nimeamua kuita vyombo vya habari ili kuhabarisha uma na watanzania wote
kwa dhumuni moja tu, la kuelezea masikitiko yangu dhidi ya Utawala huu
wa awamu ya tano, ambapo mimi Mstahiki Meya wa kinondoni, nalazimika kwa
namna moja kufanya nao kazi ya kuhudumia wananchi.
Naleta
masikitiko yangu kwenu si kwa lengo la kuchochea hasira za watu bali
kuonyesha, gilba, uzandiki, fitina na uchonganishi tunaokutana nao
kutoka kwa viongozi wa serikali ya Awamu ya tano.
Ndugu wananchi
lazma tuweke rekodi wazi ya kuwa mimi siyo mteuliwa bali mchaguliwa
kutoka kwenye kundi kubwa la viongozi mliowachagua October 2015, hivyo
mabosi wangu ni nyinyi na pakushtaki ni kwenu yani uma, ili mnitendee
sawa na mapenzi yenu mliyonituma kuwaletea maendeo.
1.KWA
MASIKITIKO SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, IMEANDIKA BARUA
KUKATAA MANISPAA YA KINONDONI TUSIPEWE MSAADA WA MRADI KIWANDA CHA
KUCHAKATA TAKATAKA ZIWE MBOLEA, KUTOKA SERIKALI YA UJERUMANI,
UNAOGHARIMU KIASI CHA SHILLINGI BILLIONI 3.2.
Kosa letu
kubwa ni msaada kutoka wakati huu ambapo manispaa ya kinondoni ina
shikiliwa na wapinzani(UKAWA) na kuonekana kwamba mradi huu ungetujenga
binafsi na siyo CCM, kukataa huku ni kwa kuandikia barua wahisani hao
kwamba mitambo na vitu vyote wanavyo panga kutuletea, vitozwe kodi,
ambayo itagharimu kiasi cha sh millioni 900.
Ikumbukwe
mradi huu ni msaada tu na siyo biashara na kwamba baada ya assembly ya
mitambo, wajerumani walikuwa wanaikabidhi manispaa ya kinondoni ndani ya
miezi 6, kitendo hiki siyo tu kutukwaza sisi kama wapinzani, ila
kimewakwaza wahisani. Wahisani hao kutoka ujerumani wamejitolea
kutusaidia billioni 3.2, ukiongeza millioni 900, tafsiri yake
tunawalazimisha watusaidie billioni 4.1, huo si uungwana hata kidogo.
Nani asiyejua
mchakato wa mradi huu ulianza sikunyingi kabla ya wapinzani kuongoza
manispaa ya kinondoni, ila mradi umekuwa hai kipindi cha wa pinzani kwa
sababu ya sifa yetu kubwa ya kutokuwa warasimu.
Ndugu wananchi hili limetusikitisha sana hasa kwa serikali hii inayo jipambanua ya kutetea wanyonge na HAPA KAZI TU.
Kushindwa
kujua kuwa mradi huu ulikuwa unakuja kufanya mapinduzi makubwa ya hali
ya USAFI si kinondoni tu bali DAR ES SALAAM yote kama jiji..
Jiji letu
lingekuwa safi na wananchi wangeondokana na michango ya takataka,sababu
mradi huu ulikuwa umelenga kutoa magari ya taka kupita mtaani
nakuzikusanya bure.
2.JUU YA UJIO WA MHESHIMIWA RAIS NDANI YA MANISPAA YA KINONDONI.
Nimeona
nilitolee ufafanuzi hili suala baada ya kuona napigiwa sana na kutumiwa
ujumbe kwa njia ya simu, watu wakitaka kujua ukweli wa mambo juu ya
lililotokea siku ya 06-09-2016.
Siku hiyo
niliomba Madiwani waliokuwa wana kikao cha kamati ya mipango miji kuja
kujumuika nasi ingawa itifaki na mpangilio wa tukio ulikuwa kichama
zaidi (Ki-ccm) kuliko kiserikali. Mimi mweneyeji kwenye manispaa yangu
wakanikalisha nyuma siti ya tatu kutoka meza kuu, huku viongozi wa CCM
kama Mwenyekiti wa Mkoa na wengine wakikaa mbele yangu.
Zaidi ni
kwamba ujio huo wa Mheshimiwa Rais sikuwa nimetaarifiwa na taasisi
yoyote ya Serikali, kuanzia Ikulu, Mkoa mpaka wilaya, isipokuwa niliona
busara kwakuwa maandalizi yaliyoendelea yalifanyikia getini kwangu, si
vyema kama muungwana kuacha kwenda kujumuika na Mheshimiwa Rais,
isingeleta picha nzuri kwa kiongozi kama mimi.
Pili,
kukosekana kwangu kwenye ratiba kusalimia au kuongea na Wananchi wangu
wa Kinondoni pia nako kulinifanya nishangae zaidi; iweje mwenyeji
nisiwepo kwenye ratiba hiyo huku watu mbalimbali wakipata fursa ya
kuzungumza ama kusalimia watu wa kinondoni.
Tatu, kupangwa
kwa mtu maalumu wa kunitukana mimi mbele ya Rais ambaye amekiri kuwa
alikutana na mkuu wa mkoa kwanza na kukubaliana kuwa ataongea huku
tayari risala kwa niaba ya wahusika ikiwa imeshatolewa.
Nne,
upotoshaji mkubwa uliofanywa na waziri Lukuvi; kwamba manispaa ionekane
tulitesa wakazi hao na kuwatapeli bila ya msaada wowote, mpaka wao
walipo amua kuja kuongea nao.
YOTE HAYA yalionyesha ni
namna
gani viongozi hawa walijipanga kumpotosha Mheshimiwa Rais na kutosema
kweli kwa dhumuni la kulaghai ama kuchafua taswira ya Manispaaa ya
kinondoni kwakuwa inaongozwa na wapinzani.
Kimsingi
Waziri Lukuvi na Mkuu wa Mkoa walikuwa na kila sababu ya kuzuia
nisipate japo dakika moja kusema ukweli juu ya mradi ule wa nyumba
kongwe magomeni kota. Mradi ule ni sawa na miradi ya wilaya zingine Dar
es salaam ambapo Temeke waliokuwa wapangaji waliondoka kwa hiari bila
kulipwa chochote wakati Ilala mpaka sasa wapangaji na manispaa wapo
mahakamani. Kinondoni pekee ndiyo ilikuwa imewalipa wapangaji wake pesa
ya kodi ili kupisha ubomoaji.
Wakati huo
wapangaji hao walikaa kwa muda wa miaka 10 bila ya umeme wala maji,
baada ya Mahakama kuamuru kuwa yalikuwa ni makazi hatarishi.
Lakini
Mheshimiwa Rais si kweli kwamba ardhi ile ilipangwa kuuzwa isipokuwa
Mheshimiwa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho kikwete alichukua baadhi ya
madiwani na kuwapeleka Indonesia ziara ya kiserikali na baadaye wakaenda
Romania, huko ndiko walipokuja na mwekezaji anayeitwa Blue Marine
kutoka Romania, ambao walikubali kuwajengea wakazi hao 644 nyumba na
kuwarudisha kama wapangaji huku wakitengeneza majengo mengine ya
biashara, makao makuu mapya ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni,
kuvunja Shule ya msingi pembeni ya magomeni kota ili kuijenga upya; Blue
Marine walikwama kungoja saini ya waiziri wa Tamisemi tangu 2014.
Na kama Rais
leo akiitisha documents hizo kutoka Tamisemi ataona mapendekeo ya
mkataba kati ya manispaa ya kinondoni na BLUE MARINE. Kusema ardhi
ilikuwa imeuzwa ni upotoshwaji mkubwa uliofanywa na waziri Lukuvi huku
akijua kuwa yeye akiwa Waziri awamu ya nne,chini ya Rais Kikwete tayari
uwekezaji wa magomeni kota likua umesha anza, isipokuwa sheria inatutaka
tumpe Waziri ili aweze kuidhinisha.
Waziri Lukuvi
kusema kuwa mradi huu ulikuwa ni wa utapeli hatukomoi UKAWA bali tuna
mshangaa kwa kumzushia shutuma hizo Rais kikwete, na akitaka kujua
ukweli wa mradi hata pale Rais alipo mtuma aje afuatilie swala hilo.
Mheshimiwa
Rais nilitaka nipate fursa nikueleze kuwa Mawaziri wote wa Ardhi walisha
wahi kutaka kupora eneo hilo. Badala ya kukutana na Halmashauri akaona
ni vema apate fursa ya kuitisha hati za Halmashauri na kuzifutilia
mbali.
Mheshimiwa
Rais kila mtu anaunga mkono juhudi za kuwasaidia wazee au wakazi wale
wa nyumba kongwe ila kupotosha umma na kuliko fanywa na Waziri kulikuwa
na lengo binafsi la kutaka kunufaika na mradi mpya utakao anzishwa.
Hasara kubwa
iliyopatikana baada ya kufutwa hati za eneo hilo ni kwamba serikali za
mitaa zimeondolewa maeneo ya uwekezaji ambayo yangesaidia kuimarisha
makusanyo ya Halmashauri na kufanya serikali hizi za mitaa ziwe tegemezi
baada ya kuporwa vyanzo vyake vya mapato. Baaada ya mwekezaji kujenga
na kuwapatia makazi wapangaji wale palikuwa na kituo kikubwa cha
uwekezaji kianzishwe.
Lakini si hilo
tu; tayari benki ya dunia walikuwa wametoa fedha za kumpatia mkandarasi
mshauri(consultant) GUff GMB kutoka ujerumani kiasi cha dola laki nne
na themanini kutuandalia michoro ya jengo la utawala kwa ajili
kuiwezesha Manispaa miongoni mwa majengo yaliyokuwa yanategemewa kutoka
kwenye mradi wa viwanja hivyo vilivyo chukuliwa.
Mheshimiwa
Rais nimalizie kuwa, ningepata walau dakika tatu ningekueleza jinsi
Waziri wako Lukuvi alivyo hatari san, na Manispaa ya Kinondoni mpaka leo
inaonja machungu yake aliyotusababishia kukosa kiasi cha shillingi
zaidi billioni ya 12, ningekufafanulia na kukuomba utumie vyanzo vyako
vya usalama kudhibitisha.
Nishukuru kuwa
hata walichopanga pia kukifanikisha uliruka kiunzi baada ya kusema
wakujenga bado haujaamua, tofauti ya Waziri Lukuvi kujiandaa na watu
wake kupokea eneo hilo, imani yangu hata kama tumeporwa bado lipo salama
sana, kuliko ungemkabidhi yeye ndiye achukue ardhi hiyo ili ekari mbili
ajenge flats za hao 644, zingine wajanja wa mjini watumie kwa mambo
yao.
Mwisho nataka
kumwambia Mheshimiwa Rais ya kuwa Wabunge, Madiwani na Mameya tunakuja
kwenye ziara zako tukijua ni ujio wa kiserikali, lakini kama kiongozi
Mkuu wa nchi tunataka uwaonye viongozi wako waache kufanya ziara zako
kuwa za kichama kuliko serikali.
Mheshimiwa
Rais usishangae Ikafika muda usituone katika ziara zako zingine kama
baadhi ya viongozi wa serikali kutaka kuchanganya uccm na ziara ya
kiserikali; au kuona mtu kama mkuu wa Mkoa akiongea vijembe kuwa eti ni
"mbabe wa vita"..ubabe dhidi ya nani? Na ni vita ipi? matusi yale mbele
yako tafsiri itakuja kuwa unawatuma au kuwapanga mapema kutoa matusi na
mipasho, sisi mameya tutaendelea kuwa ni waungwana.
Sisi Mameya wa
upinzani tumefikia mwisho, Wabunge na Madiwani kwenye ziara zako,
tukiona hatutambuliwi kama Viongozi wa Wananchi tuliochaguliwa,na
wanachi badala yake nikuona fedheha za kuita makada wa ccm watutukane.
Yaani tulienda
mbele za wananchi na kuwaomba kura kwa unyenye kevu, kama akitaka
kuonyesha ubabe basi aje agombee kata ya ubungo.
"Tumepitia
jando la kisiasa". Akiendelea kuwa kiongozi kwa kuteuliwa kamwe
asijiongopee ni mbabe, atakuwa anajilisha upepo. Na hayo yote
yanayoendelea kama yasipokemewa mapema ni wazi utakuwa unashiriki na
wakuu wa mikoa na ma DC Kuhujumu upinzani.
No comments:
Post a Comment