MAHUJAJI WA KIISLAMU KUVALISHWA BANGILI ZA KIELEKTRONIKI - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA


Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, July 1, 2016

MAHUJAJI WA KIISLAMU KUVALISHWA BANGILI ZA KIELEKTRONIKI

 
Saudia inatarajiwa kuwapatia bangili za kielektroniki mahujaji wanaoelekea katika Mji Mtakatifu wa Makka kwa ajili ya ibada ya Hajj ya mwaka huu ambayo huudhuriwa na Waislamu kutoka duniano kote.

Hatua hiyo ya kuwapa Mahujaji bangili hizo inatokana na mkanyagano uliotokea mwaka uliopita ambapo zaidi ya mahujaji 750 wanaaminikia kufariki huku wengine 900 wakijeruhiwa.

Bangili hizo zitakuwa na habari za kibinafsi za kila hujaji pamoja na zile za matibabu kusaidia mamlaka ya Saudia kuwatambua na kuwalinda mahujaji hao. Takriban kamera 1000 pia zimewekwa.



Bangili hiyo ya utambulisho itukuwa na habari muhimu kama vile pasipoti na anwani lakini pia zitatoa habari kwa mahujaji kama vile mda wa ibada pamoja na lugha tofauti ili kuwasaidia  wasiozungumza lugha ya Kiarabu wakati huo.

Bangili hizo zitakuwa haziingii maji na zitaunganishwa na programu ya ramani.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here