Afisa uhusiano wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Sebastian Mhowera akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mikakati ya Manispaa hiyo kuwawezesha wanawake na vijana kupitia mfuko maalum ulioanzishwa na Serikali ili kutoa mikopo kwa wajasiriamali hao ili kuwajengea uwezo kushiriki kujenga uchumi.kulia ni AfisaUhusiano wa Manispaa hiyo Bw.Bornwell Kapinga.
…………………………………………………………………………………………………………….
Frank Mvungi-Maelezo
Serikali kutumia zaidi ya bilioni 4 kuwawezesha wajasiriamali wadogo katika Manispaa ya Kinondoni katika Kipindi cha mwaka 2016/2017 ili kuchochea kasi ya ukuachi wa uchumi.
Kauli hiyo imetolewa Leo Jijini Dar es salaam na Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Sebvastian Mhowera wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.
Akifafanua Mhowera amesema fedha hizo zitatolewa kupitia Mfuko wa wanawake na Vijana unaolenga kuwawezesha kishiriki katika shughuli za uzalishaji hali itakayachangia kukuza uchumi.
Kwa Sasa manispaa ya Kinondoni inajumla ya Vikundi 546 vya wanawake na vijana vyenye jumla ya wajasiriamali 2729 ikilinganishwa na vikundi 40 na wanufaika 200 waliokuwepo mwaka 2013.
Wajasiriamali wanaonufaika na fedha za mfuko huo ni wale wanajishughuisha na shughuli za Kiuchumi ikiwemo kilimo, Biashara ndogondogo, Ushonaji, Ufugaji,Uvuvi,Mafundi seremala,wasusi.
Pia Mhowera alitoa wito kwa wajasiriamali wa Wilaya ya Kinondoni kujitokeza kuchangamkia fursa zinazotokana na mfuko wa wanawake na vijana.
Kuanzishwa kwa mfuko huu katika manispaa ya Kinondoni ni utekelezaji wa agizo la Serikali Kuu lililoagiza Halmashauri zote nchini kutenga asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili ya mfuko wa kuwawezesha wanawake na vijana.
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inaandaa maonesho kwa ajili ya wajasiriamali wadowadogo wanaonufaika na Mikopo ya Mfuko wa wanawake na vijana inayotolewa na Manispaa hiyo ambapo maonesho hayo yatafanyika mwishoni mwa wiki ijayo.
No comments:
Post a Comment