TANESCO YATENGA BILIONI 517 KUTEKELEZA MIRADI YAKE - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA


Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, June 23, 2016

TANESCO YATENGA BILIONI 517 KUTEKELEZA MIRADI YAKE



Na Mwandishi Wetu 

SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) limetenga zaidi  ya Sh bilioni 517 ya mapato yake kwa mwaka wa fedha 2016/2017 katika utekelezaji wa miradi yake mikubwa ikiwemo asilimia tatu wakipeleka kwa wakala wa Umeme Vijijini (REA).

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Eng. Felchesmi Mramba, fedha hizo zitalifanya shirika hilo kuwa na zaidi ya Sh bilioni  969 walizotenga kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya shirika hilo ambapo Sh.bil.449 zitatolewa na Serikali kuu pamoja na wahisani.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano wa Baraza kuu la  46 la wafanyakazi na kusema fedha hizo zitasaidia kutekeleza asilimia 50 hadi 55 ya miradi yake.
 
Mramba aliitaja baadhi ya miradi itakayotekelezwa kuwa ni pamoja na pamoja na utanuzi wa vituo vya kupoozea umeme, ununuzi wa Transfoma kubwa na mpya, utengenezaji wa njia za usambazaji umeme ambapo  kwa fedha za sasa  za mapato ya ndani zinajenga njia za umeme kutoka Mtwara na kuunganisha mkoa Lindi.

Alisema kuwa asilimia tatu ya makusanyo ya shirika hilo zinapelekwa REA  kwa ajili ya kusaidia miradi inayotekelezwa na wakala hao  ambapo katika mwaka uliopita TANESCO imechangia kiasi cha Sh. bil 50 katika miradi.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa alisema baraza hilo la wafanyakazi  lina wajibu wa kuishauri Menejimenti mambo yanayojenga na  kuleta tija katika kuhakikisha shirika linakuwa na maendeleo.
 
Katika hotuba yake iliyosomwa na Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo  Prof.James Mdoe alisema  wanapozungumzia Tanzania kuwa nchi ya viwanda ni pamoja na upatikanaji wa umeme wa kutosha.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here