BOSI WA TP MAZEMBE AHUKUMIWA JELA MIAKA MITATU - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA


Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, June 23, 2016

BOSI WA TP MAZEMBE AHUKUMIWA JELA MIAKA MITATU


KINSHASA, DRC
KIONGOZI wa upinzani wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Moise Katumbi, amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na Mahakama Kuu ya nchi hiyo kutokana na mzozo wa rasilimali, ardhi na majengo. 

Mahakama imedai kuwa Katumbi alimuuzia mtu nyumba ambayo si yake.
Kiongozi wa muungano wa vyama 15 vinavyomuunga mkono Katumbi vijulikanavyo kama G7, Kyungu Wa Kumwanza, alisema tukio hilo limepanga kudidimiza demokrasia nchini humo.

Tukio hilo limekuja katika wakati ambao Katumbi, anatarajia kugombea urais kwenye uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Novemba, Alhamisi iliyopita alifunguliwa mashtaka ya kuhatarisha usalama wa Taifa.

Kwenye taarifa iliyotolewa na Mahakama Kuu ya DRC Katumbi alishutumiwa kwa kutishia usalama wa taifa wa ndani na nje ya nchi, na alikabiliwa na waranti ya muda wa kukamatwa, Mwendesha Mashitaka wa Serikali alisema. 

Katumbi ni milionea anayemiliki timu maarufu ya soka ya TP Mazembe ya mjini Lubumbashi na Gavana wa zamani wa jimbo lenye utajiri mkubwa wa madini la Katanga. 
Adhabu ya mashitaka ya kutishia usalama wa taifa ni kifo, hata hivyo ilibadilishwa na kuwa kifungo cha maisha jela, tangu Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ilipoondoa adhabu hiyo.
Kifungo cha Katumbi kinakuja wakati ambapo kuna ongezeko la wasiwasi kutoka ndani na nje ya nchi hiyo kwamba Rais aliye madarakani, Joseph Kabila atachelewesha uchaguzi huo uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu, wakati muhula wake wa miaka mitano utakuwa unakamilika. 
Katumbi mwenye umri wa miaka 51, amekuwa hasimu namba moja wa Kabila katika kinyang'anyiro hicho cha urais, baada tu ya kutangaza nia yake ya kugombea nafasi hiyo dhidi ya kiongozi huyo wa nchi aliyehudumu kwa muda mrefu.
Mnamo  Mei 4, mwaka huu baada ya Katumbi kutangaza kuwania nafasi ya urais, mamlaka za kimahakama zilimfungulia madai ya kuwaajiri mamluki wa kigeni.
Katumbi aliwahi kuwa swahiba wa Kabila kisiasa
Katumbi alisema madai hayo, yaliyofuatiwa na kukamatwa kwa walinzi wake binafsi, ambao ni pamoja na raia wa Marekani ilikuwa ni hatua iliyoshinikizwa kisiasa.
Alipotakiwa kuzungumzia matamshi hayo ya Katumbi, Msemaji wa serikali Lambert Mende aliliambia Shirika la Habari la AFP kwamba, "anaweza kukutwa na kifungo cha nyumbani ama jela".
Wafuasi wa Kabila wanataka Uchaguzi Mkuu wa urais usogezwe mbele kwa miaka miwili kutokana na madai ya hali ngumu ya fedha na matatizo ya maandalizi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here