Na Zawadi Msalla.
………………………………….
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amekifunga mara
moja kiwanda kilicho kuwa kikiendeshwa kwa njia zisizo halali na
Wakandarasi wa Uwanja wa Taifa, Kampuni ya BFG kutoka nchini China.
Mhe.
Nape amefanya zoezi hilo leo baada ya kufanya ziara ya kukagua
maendeleo ya Uwanja wa Uhuru na kubaini kuwepo kwa kiwanda hicho ambacho
ni kinyume na taratibu na mkataba wa kisheria walio ingia baina ya
Serikali na Kampuni yao ambao unahusu ujenzi wa miudombinu ya michezo
pekee ikiwemo Uwanja wa Taifa na Uhuru.
Kabla
ya kukifungia kiwanda hicho Waziri Nape aliomba maelezo ya kina juu ya
uhalali wa uwepo wake na namna uendeshwaji wake unavyofanyika ili
kujiridhisha ndipo alipofikia uamuzi huo wa kukifungia baada ya
kujiridhisha kuwa kinaendeshwa kinyume na utaratibu.
“Ninataka
kujua kwa undani zaidi uhalali wa kiwanda hiki cha useremala kama kipo
ndani ya mkataba wa ujenzi wa Uwanja wa Taifa na eneo changamani la
michezo”. Alisisitiza Nnauye
Uwepo wa kiwanja hicho kunapelekea ucheleweshwaji wa kukamilika kwa maboresho na ujenzi wa Uwanja wa Uhuru.
Aidha
Waziri Nape amemuagiza Meneja wa Uwanja wa Taifa Rishe Urio kutoa
maelezo ya kina juu ya uwepo wa Kiwanda hicho katika eneo la ndani ya
masaa 24 ni kwanini akutoa taarifa juu ya uwepo wa shughuli za Kiwanda
hicho katika eneo hilo ila hali yeye ndiye msimamizi mkuu wa Uwanja huo.
Kwa
upande wake Meneja wa Kampuni ya BFG Cheng Longhai amekiri kuwa Kiwand
hicho kinaendeshwa kinyemela kwakuwa hakihusiani na mkataba wa kampuni
hiyo.
Wakatihuohuo
Nape ameuagiza uongozi wa Selcom Tz kuhakikisha inakimilisha mfumo wa
Tiketi za Kielekroniki na kukabidhi kwa Serikali ndani ya siku 30
kuanzia sasa.
Agizo
hilo ni muendelezo wa kutekeleza maelekezo ya Mhe. Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa Kassim wakati akiongea na wadau wa sekta ya michezo kwa mara ya
kwanza toka kuteuliwa kwake kuwa Waziri Mkuu.
No comments:
Post a Comment