Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, ametoa ushahidi
katika kesi dhidi ya Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea, akidai kwamba baada ya
kufunga mkutano na wafanyakazi wa kiwanda cha Tooku Garments, mshtakiwa
alimuita kibaka, mjinga na mpumbavu.
Akitoa ushahidi mbele
ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, jijini Dar es Salaam jana, Thomas
Simba, katika kesi ya kutoa lugha ya matusi inayomkabili Kubenea, Makonda
alidai baada ya mshitakiwa huyo ambaye ni Mbunge kupitia Chadema kumtolea lugha
ya matusi, askari polisi walimsihi asitoe lugha hiyo na kwamba hakutoa amri ya
kukamatwa kwake.
Katika kesi hiyo,
upande wa Jamhuri unaongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa
Kishenyi, akisaidiana na Wakili wa Serikali, Leonard Challo.
Akiongozwa na
Kishenyi, Makonda alidai siku hiyo alikuwa akifanya mkutano na wafanyakazi wa
kiwanda cha Tooku Garments na kwamba wakati akitangaza kuufunga mkutano huo,
alisikia sauti ya Kubenea kutoka nyuma yake ikimhoji kwanini anafunga mkutano
kabla hajaongea na wananchi wake.
“Mheshimiwa
nilipogeuka tukaonana uso kwa uso na Kubenea, akanieleza yeye ni Mbunge wa
kuchaguliwa na wananchi, aliniambia wewe ni kibaka, mjinga, mpumbavu na
umeteuliwa kwa kupewa,” alidai na kuongeza:
“Watu waliokuwapo
katika mkutano huo walimshangaa mbunge huyo kutokana na kauli zake, niliona
polisi wakimsihi kuacha kutoa lugha hiyo na aliondoka eneo la tukio hilo mara
moja.”
Baada ya Makonda
kutoa maelezo hayo, mawakili wa utetezi wa Kubenea, Peter Kibatala na John
Lyimo, walimuhoji kama ifuatavyo:
Kibatala: Ulichukua
muda gani kutoka eneo la mkutano kuingia kwenye gari lako?
Makonda: Nilichukua
dakika 10.
Kibatala: Baada ya
maneno hayo kulikuwa na taharuki gani?Makonda: Kulikuwa na hali ya sintofahamu na watu kushangaa kuona mkuu wa wilaya nikinyooshewa kidole.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
No comments:
Post a Comment