MAHAKIMU 500 KUWAJIBISHWA KWA KUKIUKA TARATIBU - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA


Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, February 2, 2016

MAHAKIMU 500 KUWAJIBISHWA KWA KUKIUKA TARATIBU

23
  






JAJI Mkuu wa Tanzania, Mohammed Othman(pichani) ametoa siku saba kwa mahakimu wakazi na mahakimu wa mahakama za mwanzo 508 kujieleza kwa nini wasifunguliwe mashtaka ya nidhamu au kuwajibishwa kwa kushindwa kufikia kiwango cha kesi walizopaswa kuamua.


Pia Jaji huyo, amekiri kuwa bado hali ya Mahakama za Mwanzo nchini ni mbaya kutokana na uchakavu wa majengo lakini pia mahakama zilizopo hazitoshelezi kulingana na mahitaji huku kukiwa na takribani wilaya 23 ambazo hazina Mahakama za Wilaya.


Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Mwaka wa Mahakama na Utendaji wa Mahakama kwa mwaka jana, Jaji Othman aliwataka mahakimu hao kuwa ni wale wanaosikiliza mashauri katika Mahakama za Hakimu Mkazi, za Wilaya na za Mwanzo.


Pamoja na kutoa siku hizo saba, aliwaagiza Majaji Wafawidhi wa Kanda kuhakikisha wanachambua na kuainisha mahakimu wote walioshindwa kufikia kiwango hicho cha kesi walizopaswa kuamua.


Alisema moja ya mikakati katika sekta hiyo ya Mahakama iliyojiwekea ni kupima utendaji wa mahakimu ili kwenda na kasi ya uwajibikaji kama ilivyo kaulimbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano ya ‘Hapa Kazi Tu.’


Alisema kwa mujibu wa mkakati huo wa kupima uwajibikaji wa kila hakimu na kila kiwango cha Mahakama, idadi ya mashauri anayopaswa kusikiliza hakimu mkazi na wa wilaya ni 250 wakati hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ni mashauri 260 kwa mwaka.


Hata hivyo, alisema kwa mujibu wa taarifa ya utendaji wa Mahakama kwa mwaka jana, imebainisha kuwa Mahakimu wakazi kwenye Mahakama za Hakimu Mkazi na za wilaya 121 waliamua mashauri chini ya 100. Aidha, alisema mahakimu wakazi na Mahakama za Mwanzo 387 waliwajibika chini ya kiwango.


“Ukiondoa wale walioajiriwa hivi karibuni, wanaofanya kwenye Mahakama za Mwanzo zisizo na mashauri mengi na wale waliokwenda masomoni au likizo za ujauzito, waliobakia wachambuliwe, waanishwe na kujieleza kwa nini hawakufikia viwango hivyo,” alisisitiza Jaji Othman.


Alisema endapo itabainika mahakimu hao hawakuwajibika ipasavyo bila sababu zozote, watafikishwa kwa Kamati ya Mkoa ya Nidhamu na Maadili ya Hakimu na kufunguliwa mashtaka ya nidhamu na mashtaka hayo yatashughulikiwa haraka na Kamati za Maadili za Mahakama.


BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here