Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Dila Africa, Jumba Dickson akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi wa ufugaji sungura, wakati waandishi hao walipotembelea kwa mmoja wa wafugaji wa sungura hao katika eneo la Kivungwi, Kata ya Vigazwa Mkoa wa Pwani. KATUMA BLOG tz
Dickson akizuingumza na waandishi wa habari waliokuwa kwenye ziara ya mafunzo kuhusu mradi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Dila Africa Co. Ltd Jumba Dickson (kushoto) akiwa amebeba mmoja wa Sungura wanaofungwa kupitia mradi huo. Kulia ni Gladness Nyange Mjasiriamali anayejihusisha na ufugaji wa Sungura.
Gladness Nyange na Jumba Dickson wakiwaonesha waandishi wa habari sungura hao wanaofugwa kupitia mradi wa ufugaji Sungura, nyumbani kwa Gladness.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakitembelea katika mabanda yanayotumika kuwafugia Sungura hao.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakitembelea katika mabanda yanayotumika kuwafugia Sungura hao.
Dickson akifafanua jambo kuhusu mradi huo mbele ya waandishi wa habari.
Na Katuma
Masamba, KATUMA BLOG tz
WATANZANIA
wameshauriwa kujihusisha na ufugaji wa sungura ili waweze kujiongezea kipato
kutokana na mnyama huyo kuwa na faida nyingi.
Faida
wakulima wanazoweza kupata kutokana na mnyama huyo mbali na kuuza nyama yake
lakini pia wanaweza kuuza kinyesi, mkojo pamoja na ngozi yake.
Ushauri
huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Dila Africa, Jumba Dickson
wakati akizungumza na waandishi wa habari waliokuwa katika ziara ya mafunzo
kuhusu mradi huo juzi katika eneo la Kivungwi kata ya Vigwaza, Mkoani Pwani.
Dickson
alisema, ufugaji wa sungura unaweza ukawasaidia wakulima katika kujiongezea
kipato kwa mbali na kuuza nyama yake lakini pia wana uwezo wa kuuza kinyesi,
mkojo pamoja na ngozi yake.
“Tunawafundisha
wakulima jinsi ya kufuga sungura ili waweze kunufaika, lakini wanaweza
kujiuliza ni wapi wanaweza kuwauza wakishafikia hatua ya kuuzwa, sisi tunawapa
soko kwa hiyo kikubwa kwa mkulima ni kufuga tu,” Dickson alisema.
Alisema
kampuni yake ina mashamba ya sungura hivyo wanapoingia mkataba na wakulima
wanaohitaji kufuga wanakubaliana mambo mbalimbali ikiwemo kuwatafutia masoko
ambapo wao wenyewe wananunua sungura hao.
Naye
Mjasiriamali na mfugaji wa sungura hao, Gladness Nyange alisema, kuna umuhimu
wa akinamama kutumia fursa ya ufugaji sungura ili kumudu kuwasomesha watoto wao
badala ya kuwategemea waume zao.
Alisema
licha ya kuwa sungura hao wanahitaji uangalizi wa hali ya juu katika kuwafuga
lakini amekuwa akihakikisha kuwa waishi katika mazingira mazuri ili waweze
kumpa faida.
“Huu ufugaji
kwa kuwa ni mpya watu, wengi wanaweza kujiuliza inakuwaje au masoko watapata
wapi...lakini mimi nilipoanza kufuga niliingia mkataba na hii kampuni na wao
walinipa masoko ina maana kwa kila sungura wa kilo nne nauza kwa Sh 40,000,”
Nyange alisema.
Nyange
alishauri wajasiriamali na hasa wanawake kujiingiza katika ufugaji huo ili
waweze kufanya mambo yao mbalimbali bila kuwategemea akinababa ambao wakati
mwingine wanakuwa na majukumu memgi
No comments:
Post a Comment