Na Magreth Kinabo- MAELEZO
Serikali imesema kwamba tamko lake
lilitolewa hivi karibuni kuhusu matangazo ya Tiba Asili na Tiba Mbadala
palepale kwa kuwa lengo lake ni kuboresha huduma hiyo. Hivyo kama kuna mtoa huduma ambaye amekwazika na tangazo
hilo ipo tayari kuzungumza naye.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tamko hilo kwenye ukumbi wa mikutano
wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
Tamko hilo ambalo lilitolewa Desemba 24, mwaka huu,ambapo limepiga
marufuku matangazo yote yanayohusu tiba asili na tiba
mbadala kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Ambapo kwa wale wenye vibali
wanatakiwa kuviwasilisha vibali na matangazo yao kwenye Baraza la Tiba Asili na
Tiba Mbadala ili vifanyiwe mapitio.
Tamko hilo liliendelea
kufafanua kwamba utoaji wa elimu
ya afya kwa umma unaofanywa na watoa huduma za tiba asili na tiba mbadala
kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii umepigwa marufuku hadi hapo
utaratibu mwingine utakapotangazwa.
‘Watoa huduma za tiba asili na tiba
mbadala nchini kote wanaagizwa wawasilishe kwenye Baraza nyaraka zote muhimu
ndani ya wiki mbili kuanzia leo Desemba 2015. Baadhi ya nyaraka hizo ni zile
zinazohusu kuuza dawa za asili na tiba mbadala, nyaraka za kumiliki mashine
zinazotumika katika kufanya uchunguzi katika tiba asili na tiba mbadala,’
lilieleza tamko hilo.
Tamko hilo lilifafanua kwamba Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala
linaagizwa katika kipindi cha siku 14 kuanzia leo 24 Desemba 2015, lipitie
nyaraka zote zikapowasilishwa zinazohusu usajili wa watoa huduma, usajili wa
vituo vyao, ikiwa ni pamoja na maduka ya dawa za asili na dawa za tiba mbadala,
usajili wa dawa zote zinazotumika katika huduma hizo na usajili wa mashine zote
zinazotumika katika huduma za tiba asili na tiba mbadala.
Aidha akizungumzia kuhusu tangazo hilo, Waziri Ummy alisema ‘Mimi
niko tayari kuzungumza na mtoa huduma ambaye amikwazika na tangazo hili,
ili aweze kueleza ni sababu zipi zinazomfanya asisajiliwe. Tunafanya hivi kwa mujibu wa sheria ,kanuni
na taratibu,’ alisisitiza.
Aliongeza
kwamba Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala Namba 23 ya Mwaka 2002 inaeleza wazi.
Kwa mujibu wa Waziri huyo alitaja idadi ya
watoa huduma hiyo kuwa ni wako 75,000
kwa takwimu za nchi nzima.Naye
Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba
Mbadala, Dkt. Edmund Kayombo alisema hadi sasa hawajapokea mrejesho wa tamko la
tamko hilo la Serikali.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Shirikisho la
Vyama Vya Tiba Asili
Tanzania(SHIVYATIATA), Abdulrahaman
Lutenga alisema hakuna mganga
yoyote aliyepinga tamko hilo na Serikali, hivyo tamko lililotolewa hivi karibuni la kupinga
agizo hilo si halali kwa kuwa halikupitia katika shirikisho hilo.
‘
Hatutambui kampuni hii iliyotoa tamko la kupinga tangazo la Serikali kwani ya
mtu binafsi yenye wanahisa 11,’ alisema Lutenga.Akizungumzia kuhusu hatima ya tamko hilo, Dkt. Kayombo alisema baada ya
siku walizotoa kumalizika watatangaza hatua zipi zitachukuliwa kama vile
kuwaondoa wasiofuata sheria.
No comments:
Post a Comment