RAIS DK.JOHN MAGUFULI ATOA ZAWADI YA KRISMAS NA MWAKA MPYA KWA WATU WALIO KATIKA MAKUNDI MAALUMU JIJINI DAR ES SALAAM LEO - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA


Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, December 23, 2015

RAIS DK.JOHN MAGUFULI ATOA ZAWADI YA KRISMAS NA MWAKA MPYA KWA WATU WALIO KATIKA MAKUNDI MAALUMU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

  Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Rabikira  Mushi(katikati), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wakati akikabidhi zawadi ya Chrismas, Mwaka mpya kwa watu walio katika makundi maalumu kwa niaba ya Rais Dk.John Magufuli. Kulia ni Kamishna Msaidi wa Ustawi wa Jamii, Beatrice Fungamo na kushoto ni Msemaji wa Wizara hiyo, Nsachris Mwamwaja.
 Viongozi kutoka Ustawi wa Jamii na wageni waalikwa na wanahabari wakiwa katika mkutano wa makabidhiano hayo.
 Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Rabikira  Mushi (kushoto), kwa niaba ya Rais Dk.John Magufuli akimkabidhi mbuzi na vyakula Ofisa wa Ustawi wa Jamii, Happynes Nyange wa Makao ya Taifa ya watoto Yatima Kurasini kwa ajili ya Sikukuu za mwishoni mwa mwaka na mwaka mpya Dar es Salaam leo asubuhi.


Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Rabikira  Mushi (kushoto), kwa niaba ya Rais Dk.John Magufuli akiwakabidhi mbuzi na vyakula, Watawa wa Kituo cha Mother Theresa cha  Mburahati jijini Dar es Salaam.
Mbuzi akiingizwa kwenye gari baada ya kukabidhiwa kwa wahusika.

Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Rabikira  Mushi (kushoto), kwa niaba ya Rais Dk.John Magufuli akiwakabidhi mbuzi na vyakula, Veronica Msanjila wa Makao ya Wazee na wasiojiweza  Nunge Kigamboni jijini Dar es Salaam.

 Na Dotto Mwaibale

RAIS wa awamu ya tano Dk. John  Magufuli,  ametoa zawadi  ya vyakula, mbuzi na mafuta ya kupikia zenye  thamani   ya Sh  mil  8,089, 000  kwa watu walio katika makundi  maalum wakiwemo watoto wanaoishi katika  mazingira hatarishi,watu wenye ulemavu pamoja na wazee.

Akikabidhi msaada huo katika kituo cha kulelea watoto wanaokinzana na sheria kilichopo Upanga jijini Dar es Salaam, kwa niaba ya Dk. Magufuli, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Rabikira  Mushi,  alisema katika kusheherekea sikukuu za maulid,Chrismas  na mwaka mpya Dk Magufuli ameamua kutoa zawadi katika vituo nane  katika mkoa wa Dar es Salaam , viwili  Zanzibar na Vituo Vitano toka mikoani kwa Tanzania Bara.

Alitaja vituo hivyo kuwa ni  Makao ya Taifa ya watoto yatima Kurasini,mahabusi ya watoto Upanga kilichopo Ilala,Makao ya Wazee na wasiojiweza  Nunge Kigamboni,Chuo  cha Ufundi kwa watu wenye ulemavu Yombo, Kituo cha Mother Theresa  Mburahati  Kinondoni,Kijiji cha Furaha Mbweni kilichopo Kinondoni, Dar al arqum Tandika (Temeke) na kituo cha watoto Msimbazi, Kwa Zanzibar  kituo cha Maboani Chakechake Pemba  na Cha wezero Unguja.

Alisema kwa mikoa ya Tanzania  Bara  vituo vilivyopatiwa msaada ni Makao ya watoto Kemondo(Bukoba), Kituo cha Village of Hope(Dodoma),Shule ya maadirisho Irambo(Mbeya), Makazi ya wazee wasiojiweza Bukumbi,Misungwi(Mwanza) na Makazi ya wazee wasiojiweza Sukamahela, Manyoni, (Singida).

“Lengo la Dk. Magufuli  kutoa zawadi hiyo ni kuwawezesha makundi hayo   ya weze kusheherekea  sikukuu kama ilivyo kwa watu wengine.”alisema Mushi.

Meneja wa mahabusu ya watoto Upanga, Ramadhani Yahaya alisema wanamshukuru rais Dk. Magufuli kwa ukarimu wake hasa kuwakumbuka watoto wa ukinzani wa sheria na kudai kuwa mara nyingi wadau  wamekuwa hawawakumbuki.

“Tunawaomba wadau wengine wawe na moyo wa kuwasaidia watoto hawa, pia tuna matatizo ya ufinyu wa bajeti katika serikali kunahuduma muhimu ambazo tunazikosa  tunaomba wadau mbalimbali wajaribu kusaidia kutujengea uzio  kwakuwa serikali itachukua muda kutatua tatizo hilo”.alisema Mushi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here