Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchanguzi Jaji Msitafu Damian Lubuva akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya majina ya wabunge wa Viti Maalum yatapatikana katika Vyama husika kwa mujibu wa Orodha iliyowasilishwa Tume na kila Chama ila Tume (NEC)iweze kufanya Uteuzi, kikao hicho kimefanyika leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Emmanuel Kavishe.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Msitafu Damian Lubuva
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza Viti Maalum vya Wabunge 110 kwa vyama vitatu ambavyo vimevuka asilimia tano ya kura za wabunge.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu, Damian Lubuva amesema idadi ya wabunge imeongezeka kwa kufikia asilimia 40 kutokana na uamuzi wa serikali wa mwaka 2010 kwa kuongeza idadi ya viti maalum vya wanawake.
Lubuva amesema kutokana na kuwepo majimbo ya nane ambayo hayakufanya uchaguzi kunafanya viti vitatu kutokuwepo, baada ya uchaguzi wa majimbo hayo viti vitarudi kwa vyama.
Katika mgawanyo wa viti maalumu vya wanawake katika bunge linalotarajiwa kuanza hivi karibuni Chama cha Mapinduzi (CCM), kimepata viti 64, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) viti maalum 36 na Chama cha Wananchi (CUF) Viti Maalum 10.
Majina ya viti maalum yatapatikana katika vyama husika kwa mujibu wa orodha iliyowasilishwa Tume ya kila chama ili tume iweze kufanya uteuzi.
No comments:
Post a Comment