Mkuu
wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC), Giveness Aswile, akizungumza katika mkutano na waandishi wa
habari Dar es Salaam leo, kuvishukuru vyombo vya habari kwa kuripoti
vizuri katika kipindi chote cha uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani.
Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NEC, Emanuel Kavishe.
Kavishe naye akitoa pongezi kwa wanahabari kwa kutangaza vizuri matukio ya uchaguzi mkuu
Sehemu ya wanahabari wakiwa katika mkutano huo
Aswile na Kavishe wakifurahia jambo katika mkutano huo.
Lilian Lundo-MAELEZO
TUME
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa mafanikio ya asilimia 80 ya
uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 yametokana na ushiriki mkubwa wa vyombo vya
habari vilivyotekeleza kwa ufanisi kazi ya kuelimisha na kutoa habari
kuhusu uchaguzi huo.
Akiongea
na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa tume hiyo, Mkuu wa
Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga kura Giveness Aswile, amevishukuru
vyombo vya habari kutokana na kazi hiyo katika kipindi chote cha
uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani.
Alisema
amani ya Tanzania iliendelea kuimarika katika kipindi chote cha
uchaguzi kwa sababu vyombo vya habari vilisimamia na kutetea haki za
wananchi.
Aliongeza
kuwa hata tume ilifanya kazi kwa urahisi kutokana na kazi kubwa ya
uelimishaji iliyofanywa na vyombo vya habari, hivyo kuipunguzia kazi NEC
ya kuwaelimisha wananchi juu ya mambo ya msingi ya uchaguzi mkuu.
“Amani
ya nchi hii ilisimama kwa sababu vyombo vya habari vilisimama kutetea
wananchi na tume, ilifika mahali maswali kutoka kwa wananchi yalipungua
kutokana na maswali mengi kujibiwa kupitia vyombo vya habari” Alisema
Giveness.
Naye
Mkurugenzi Idara ya Sheria wa tume hiyo, Emmanuel Kawishe alisema
hakuwa na ufahamu sahihi kuhusu vyombo vya habari na umuhimu wake katika
kutekeleza majukumu yake kwa wananchi.
“Zamani
nilifahamu mwanahabari ni adui kumbe ni daraja kati ya mtoa habari na
mpokea habari, katika zoezi zima la uchaguzi mkuu wanahabari walikuwa ni
sehemu ya waliotoa elimu ya mpiga kura wameweza kutumia kalamu zao
vizuri.” Alisema Bwana Kawishe
Alifafanua
kuwa wanahabari walifanya kazi yao kwa kuzingazitia maadili ya kazi yao
kwa kutofungamana na upande wowote na kuitangaza tume kwa mtazamo
chanya kwa wananchi.
Kawishe
alisema kuwa vyombo vimeweza kuitangaza vizuri tume kwani kila
alipopita wananchi wamekuwa wakiipongeza NEC kwa kazi nzuri ya utoaji wa
elimu ya mpiga kura katika vyombo vya habari.
Uchaguzi
Mkuu wa mwak 2015, umeshuhudia ushirikishwaji mkubwa wa vyombo vya
habari ambapo vyombo vya habari vilipewa nafasi kubwa ya kutoa habari
kuhusu uchaguzi huo ikiwemo kutoa vitambulisho vilivyowaruhusu waandishi
wa habari kuingia kwenye vituo vya kupigia kura.
No comments:
Post a Comment