Dr
Alok Ranjan, mtaalamu wa magonjwa ya mfumo wa fahamu na uti wa mgongo
kutoka hospitali ya Apollo akitoa huduma kwa mtoto Zulea akiwa na mama
yake Shamila Idd katika kliniki iliyofanyika siku
tatu.’
Dr
Alok Ranjan, mtaalamu wa magonjwa ya mfumo wa fahamu na uti wa mgongo
kutoka hospitali ya Apollo akiongea na waandish wa habari katika cliniki
iliyoanza tarehe 11 na kuendelea mpaka tarehe 13 katika hospitali ya
Hindumandal.
Bwana
Hafidhi Rashid Waziri, mmoja wa wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa uti
wa mgongo na Dr Alok Ranjan katika hospitali ya Apollo Hyderebad
akiongea na waandishi wa habari katika Klinik hiyo.
Shamila
Idd mama wa mtoto Zulea mwenye tatizo la uti wa mgongo akiongea na
waandishi wa habari katika kliniki iliyoandaliwa na Dr Alok Ranjan,
mtaalamu wa magonjwa ya mfumo wa fahamu na uti wa mgongo kutoka
Hospitali ya Apollo.
Na Mwandishi Wetu,
Tanzania
ni moja ya nchi ambazo ina uhaba mkubwa wa madaktari bingwa wa mfumo wa fahamu
kitendo kinachopelekea nchi kupoteza fedha nyingi kwa kuwapeleka wagonjwa wa
matatizo ya aina hiyo nje ya nchi kupata matibabu na ushauri.
Inakadiriwa
kuwa watoto wachanga 1000 kati 4000 wanaozaliwa na tatizo la mfumo wa fahamu
hupatiwa matibabu huku wengine 3000 wakishindwa kupatiwa matibabu.
Kutokana
na hali hiyo, Hospitali ya Apollo ya nchini India imemleta nchini daktari
bingwa wa upasuaji wa uti wa mgongo na mfumo wa fahamu ambaye pia ni Mkuu wa
idara ya upasuaji wa magonjwa ya fahamu katika hospitali hiyo
DKT ALOK RANJAN ambaye atakuwa akitoa huduma na kuwaona wagonjwa wake aliowafanyia upasuaji siku za nyuma.
DKT ALOK RANJAN ambaye atakuwa akitoa huduma na kuwaona wagonjwa wake aliowafanyia upasuaji siku za nyuma.
Nao baadhi
ya wagonjwa waliofika katika kliniki hiyo inayofanyikia katika hospitali ya
hindu mandal jijini Dar es Salaam wameiomba serikali kuhakikisha kwamba
inasaidia katika gharama za matibabu ya watu wanaosafiri nje ya nchi kufuata
matibabu ya magonjwa mbali mbali.
Wamezitaka
pia kampuni za bima ya afya kuhudumia wateja wake katika hospitali za kimataifa
badala ya kujikita katika hospitali za hapa nchini pekee.
Katika mkutano huo na waandishi wa
habari ulofanyika tarehe 12 katika hospitali ya hindumandali Dk. Alok Ranjan kutoka Hospitali
za Apollo amewashauri watanzania kubadilisha mtindo wa maisha ili kuepukana
na magonjwa ya mfumo wa fahamu na uti wa mgongo. anasema kuwa kwa watu wazima
ugonjwa huu mara nying husababishwa na namna mbovu ya ukaaji ambao hudhuru uti
wa mgongo, trauma, shinikizo la damu, ajali, kisukari, uzito wa kupitiliza na
sababu nyinginezo.
Tanzania
kwa sasa inakadiriwa kuwa na madaktari wa mfumo wa fahamu 7 ambao wote kwa sasa
ni watendaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment