Na Woinde Shizza,Arusha.
Mgombea
ubunge wa jimbo la Arusha kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Philemon Mollel
amewataka wakazi wa jiji la Arusha kumchagua kwa kura za kishindo kwani anatosha
kuliongoza jimbo la Arusha na jiji hilo si sehemu ya kujinadi kwa
mapambao bali kuwalete wananchi
maendeleo.
Mollel
ameyasema
hayo wakati alipokuwa akijitambulisha na kuomba kura kwa wakazi wa
kata ya Levolosi na kuwataka kuendelea kukiamini chama cha mapinduzi
pamoja na yeye
kwani anatosha kuliongoza jimbo la Arusha Mjini, wakati chama hicho
kijiandaa kuanza kampeni zake hapo Jumamosi ijayo mgombea apita kwenye
mashina kuomba kura.
Alisema kuwa
anaomba kura kwa wanachama na wasiokuwa wanachama kwani
maendeleo hayana
itikadi za vyama vya siasa hivyo akawataka kumtuma naye awe mtumishi wa
wananchi wa jimbo la Arusha mjini.
“Mnajua
siendi kuganga njaa bungeni bali naenda kupeleka kero zenu na nani uchungu na
maendeleo ya kinamama,wazee na vijana kwani nitaanzisha saccos kwa kila kata
ilimpate mikopo ya kujikwamua na kuweza kujiletea maendeleo”alisema
Mollel.
Aliwataka
wakereketwa na wale wafuasi wa vyama vingine kuweka pembeni ushabiki na
kumchagua yeye ilikuirudiisha Arusha kuwa Giniva ya Afrika na kuirudisha Arusha
yenye amani na kuweza kurudisha sifa ya jiji
hilo.
Awali
akimkaribisha Mgombea kwa wanachama na wafuasi wa chama hicho sanjari na
wananchi Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Arusha Dkta Soiley amewakata
kuacha ushabiki wa kisiasa na kumchagua Mollel kwani anatosha
kuliongoza jimbo la
Arusha.
Soiley
alisema
kuwa pamoja na kupigwa katika uchaguzi mkuu kwa nafasi za udiwani mda
umefika kwa kumchagua Philemon Mollel kuweza kuiletea maendeleo na
kudumisha sifa ya jiji la Arusha ya kuwa na Amani na kivutio cha utalii
kwani uchaguzi ulipita na sasa ni wakati wa kuunganisha nguvu na kumpa
kura za kishindo mgombea wa chama hicho.
“Nawasihi
ndugu zangu kutafuta wanachama kumi kwa kila mtu ilikuunganisha nguvu na kuipa
ccm ubunge wa jimbo letu kwani nyinyi ni mashahidi wakubwa hakuna
kilichofanyika katika kuwaletea wananchi maendeleo kwa mda wa mbunge
aliyemaliza mda wake kwa kipindi cha miaka
mitano”alisema Soiley.
No comments:
Post a Comment