Wakulima
wametakiwa kutumia vizuri dhamana waliyopewa ya ya mfumo wa vocha ili
kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara kwa maslahi yao na
Taifa kwa ujumla.
Wito
huo umetolewa jijini Dar-Es-Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano,
Wizara ya Kilimo, Chakula na Viwanda Richard Kasuga alipokuwa akitoa
taarifa ya ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa njia ya vocha nchini.
Kasuga
aliendelea kusema kuwa matumizi sahihi ya mbegu bora na mbolea kwa
mfumo wa vocha kunaongeza uwezo wa Taifa kujitosheleza kwa chakula ili
kuondokana na umaskini na kufanikisha mapinduzi ya kijani.
“Vocha
ni haki ya mkulima na siyo upendeleo kwa mkulima anayepatiwa pembejeo
hizo, hivyo itumike ipasavyo ili kuongeza uzalishaji wa mazao husika na
kuleta tija katika mazao ya mahindi na mpunga” alisema ndugu Kasuga.
Katika
utaratibu huo wa vocha, wakulima wa mahindi na mpunga hunufaika kwa
kupatiwa pembejeo, ambazo ni mbegu bora na mbolea zinazotosheleza ekari
moja ambapo Serikali inachangia asilimia 50 ya bei ya soko kwa kila aina
ya pembejeo wanayopewa wakulima hao.
Vigezo
vinavyotumika kutoa ruzuku kwa wakulima nchini ni pamoja na mnufaika
kuwa na makazi ya kudumu katika kijiji na awea analima mpunga au mahindi
na kaya iwe tayari kusaini hati ya pembejeo ili itumie kanuni ya kilimo
bora.
Kigezo
kingine ni kaya kuwa na eneo lisilopungua ekari moja pamoja na kaya
zinazoongozwa na makundi maalum hususani wajane na walemavu ndiyo hupewa
kipaumbele.
Akizungumzia
faida za mfumo huo wa vocha, ndugu Kasuga alisema kuwa ni pamoja na
kuongezeka kwa uzalishaji wa chakula, ambapo ongezeko hilo limewezesha
wakulima kuuza chakula ndani na nje ya nchi hivyo kuinua hali zao
kiuchumi.
Aidha,
Taifa limeondokana na tatizo la kuagiza chakula nje ya nchi jambo
ambalo limesaidia kuokoa fadha za kigeni hali inayotokana na elimu bora
iliyotolewa kwa wakulima ambao wamehamasika kutumia mbegu bora na mbolea
kwa maendeleo endelevu ya kilimo.
Utaratibu
wa kutoa ruzuku ya pembejeo kutoka Serikalini kwa mfumo wa vocha
ulianzishwa na mwaka 2008/2009 ili kuboreka mfumo wa namna ya
kuwafikishia wakulima ruzuku ya mbegu bora na mbolea ambazo hazikuwa
zikiwafikia wakulima walengwa watarajiwa kwa namna iliyotarajiwa.
Ili
kuendeleza kilimo chenye tija, makampuni 23 ya mbolea na 27 ya mbegu
bora ya mahindi na mpunga yanaendelea kutoa huduma ya kusambaza pembejeo
hizo katika mikoa inayolima mazao hayo.
No comments:
Post a Comment