Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes nchini Naigeria, Bw. Jack Liu (wa pili kulia) akiwa ameshikilia sare ya kampuni hiyo pamoja na mabalozi wapya Jonathan Akpoborie (wa kwanza kushoto) na Kanu Nwankwo (katikati) wakati wa hafla fupi ya kuwatambulisha mabalozi wapya wa kampuni hiyo jijini Lagos Naigeria mwishoni mwa wiki. Wakijumuika kwa pamoja katika tukio hilo ni wafanyakazi wa kampuni hiyo nchini Naijeria Bw. Maxwell Loko na Dare kafar (wa kwanza kushoto).
Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes nchini Nigeria, Bw. Jack Liu (wa pili kulia) akiwa ameshikilia sare ya kampuni hiyo pamoja na mabalozi wapya Jonathan Akpoborie (wa kwanza kushoto) na Kanu Nwankwo (katikati) wakati wa hafla fupi ya kuwatambulisha mabalozi wapya wa kampuni hiyo jijini Lagos, Nigeria mwishoni mwa wiki. Wakijumuika kwa pamoja katika tukio hilo ni wafanyakazi wa kampuni hiyo nchini Naijeria Bw. Maxwell Loko na Dare kafar (wa kwanza kushoto).
Na Mwandishi Wetu, Nigeria
Katika kuhakikisha huduma za dijitali zinafurahiwa na zinamfikia kila mtu, kampuni ya StarTimes imeingia makubaliano na aliyekuwa mchezaji nguli wa kimataifa wa soka wa Nigeria, Nwankwo Kanu kama balozi wa shughuli zake barani Afrika.
Akizungumzia juu ya ushirikiano huo Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes nchini Tanzania, Lanfang Liao amebainisha kuwa, “Mkataba baina yetu na Kanu ulitiwa saini jijini Lagos nchini Nigeria ambako Kanu alikubali kuingia mkataba kwa miaka mitatu. Hivyo basi balozi wetu huyu mpya atakuwa muwakilishi wa kampuni yetu yenye shughuli zake takribani nchi 12 barani Afrika zikiwemo Nigeria, Tanzania, Kenya, Uganda, Afrika ya Kusini, Msumbiji, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na nyinginezo.”
Kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba huo, Kanu sasa atakuwa akishiriki katika shughuli kama vile matangazo, kuhudhuria sherehe za kampuni, matukio na kusaidia kukuza muonekano wa StarTimes barani Afrika pamoja na hamasa kwa watu kuhamia katika mfumo wa dijitali.
Kanu pia atakuwa akisaidiana na aliyekuwa mchezaji wa kimataifa wa soka wa Nigeria, Jonathan Akpoborie ambaye yeye pia ameteuliwa kuwa mtaalamu wa kupanga vipindi vya michezo na mgeni mwalikwa katika uchambuzi wa vipindi vya moja kwa moja. Akpoborie atakuwa akishiriki kama mchambuzi wa kiufundi wa vipindi vya moja kwa moja vya michezo vitakavyokuwa vikirushwa katika chaneli za StarTimes vikionyesha uchambuzi na makala yakinifu.
Jonathan Akpoborie ni mchezaji wa zamani wa kimataifa kutoka nchini Nigeria ambaye alitumia muda wake mwingi kucheza soka la kulipwa nchini Ujerumani.
Akifafanua umuhimu wa kumchagua Nwankwo Kanu kama balozi wa StarTimes Afrika, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu huyo nchini Tanzania amesema kuwa StarTimes ilizingatia sana la mtu ambaye anakaubalika si tu nchini mwake bali katika bara zima la Afrika.
“Ukiachilia mbali mafanikio aliyoyapata Kanu katika medali za kimatifa, umaarufu wake haupo tu nchini kwake Nigeria bali katika bara zima la Afrika. Kanu ni hamasa ya kweli katika historia ya mafanikio ya wanasoka kutoka Afrika kwa kufikia mafanikio makubwa licha ya mazingira magumu. Ni mfano wa kuigwa ambaye kila mtu anaweza kumtazamia kufikia ndoto zake.” Alisema Liao
Aliongezea pia, “Wakati dunia tayari imekwishahama kutoka kwenye mfumo wa analogia, StarTimes inawekeza vya kutosha, kukusanya rasilimali na kuwahusisha wadau ili kuhakikisha waafrika wanaingia katika mfumo mpya wa matangazo ya luninga kwa dijitali na kuwaunganisha na ulimwengu kwa ujumla. Tunapigania kuwaunganisha watu wengi zaidi, kuwahamasisha na kuwapatia msisimko wateja wetu kote barani Afrika kuhusiana na matangazo ya dijitali.”
Naye kwa upande wake akiwa mwenye furaha Nwankwo Kanu aliishukuru kampuni ya StarTimes kwa kumuona anastahili kuwa balozi wa kampuni hiyo.
“Ninayo furaha kubwa sana kusaidia kukuza na kuunga mkono shughuli za StarTimes kama balozi wake barani Afrika. Lengo langu ni kuhakikisha kila mwafrika amekuwa amehamia katika matangazo ya dijitali ifikapo mwezi Juni 17, 2017 na nimefurahi kushirikiana na StarTimes katika kulifanikisha hili.” Alisema Kanu
“Ukiachana na kuwa kapteni mstaafu wa kikosi cha Super Eagles cha Nigeria, Kanu ni mchezaji wa kiafrika mwenye mafanikio lukuki yakiwemo, kushinda medali ya UEFA Klabu Bingwa barani Ulaya, medali ya kombe la UEFA, medali tatu za washindi wa kombe la FA na tunzo mbili za mchezaji bora barani Afrika hizo zikiwa chache tu zilizoorodheshwa. Pia ni mchezaji wa kipekee kuchezea soka la ligi ya Uingereza kushinda vikombe vya EUFA Kilabu Bingwa barani Ulaya, kombe la UEFA, ligi kuu Uingereza, kombe la FA na medali ya dhahabu ya Olimpiki.” Alihitimisha Liao
Kanu pia atakuwa akishiriki kwenye uchambuzi wa kina pamoja na wapenzi wa soka kama mgeni rasmi katika matangazo ya moja kwa moja ya mechi za ligi za Bundesliga na Serie A zinazorushwa mahususi katika chaneli za StarTimes.
StarTimes kwa sasa inayo hakimiliki za kurusha moja kwa moja mechi za ligi za Bundesliga (Ujerumani), Serie A (Italia) na Ligue 1 (Ufaransa). Na kwa sasa inarusha moja kwa moja michuano ya FIFA kombe la dunia la vijana chini ya miaka 17 iliyoanza kutimua vumbi Oktoba 18 na kumalizika Novemba 8 nchini Chile.
No comments:
Post a Comment