Uchafuzi wa mazingira katika vituo vya vivuko ,
utegaji wa nyavu katika njia za vivuko na kukauka kwa maji na kujaa mchanga
kwenye njia za vivuko ni sababu zinazochangia kuharibika kwa vivuko nchini.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa
Ukodishaji mitambo na Huduma za Vivuko kutoka
wakala wa Ufundi wa umeme Tanzania Mhandisi Japhet Maselle.
Aidha, alitaja
sababu za uharibifu wa vivuko hivyo kuwa ni pamoja na baadhi ya abiria
kutofuata taratibu za vivuko na wananchi kutumia mitumbwi ambayo si salama
kuvukia hasa maeneo ya magogoni Dar es salaam na Pangani Tanga .
“Utegaji wa nyavu husababisha kunasa kwenye mifumo
ya kuendeshea vivuko, na takataka kuingia kwenye mitambo ya kuendeshea vivuko
ambapo husababisha athari katika mitambo
hiyo” alisema ndugu Maselle.
Katika kukabiliana na matatizo hayo, TAMESA
imeendelea kutoa elimu kwa watu wanaochafua mazingira na maeneo ya vivuko
kutangaza taratibu za vivuko ndani ya vivuko
na kuboresha huduma za vivuko na
kuongeza maeneo yenye uhitaji.
Wakala wa ufundi na Umeme Tanzania (TAMESA)
ilianzishwa kwa sheria ya wakala namba 30 ya mwaka 1997 ikiwa na lengo la kutoa
huduma katika Nyanja za uhandisi mitambo, umeme na uendeshaji wa vivuko .
Kwa sasa kuna vivuko 28 vinavyofanya kazi katika
vituo 19 Nchini, baadhi ya vivuko hivyo ni Mv Msungwi,Mv sabasaba, Mv
Sengerema,Mv mwanza, Mv ukara , Mv Nyerere na Mv Temesa.
No comments:
Post a Comment