Ofisa Mtendaji wa Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasco), Mhandisi Cyprian Luhemeja, akizungumza katika mkutano na wafanyakazi uliofanyika hivi karibuni Makao Makuu ya Dawasco jijini Dar es Salaam kuhusu utendaji kazi wa kazi.
Wafanyakazi wa Dawasco wakimsikiliza Ofisa Mtendaji
Mkuu wao.
Na Mwandishi, Maalumu
Ule usemi maaarufu wa Hapa kazi tu”unaendelea kuimbwa na
kufanyiwa kazi na Watanzazia wengi hususani watumishi wa Umma na Serikali ili
kuendana na kasi ya awamu ya Tano ya Raisi John Magufuli.
Kauli mbiu hiyo imekumbushwa tena na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Eng Cyprian Luhemeja wakati wa kikao cha pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo mapema wiki hii.
Kauli mbiu hiyo imekumbushwa tena na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Eng Cyprian Luhemeja wakati wa kikao cha pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo mapema wiki hii.
“Lazima tuendane na kasi ya Mheshimiwa Rais, tabia ya
kufanya kazi kwa mazoea, kutojali malalamiko ya Wateja sasa ni mwisho” Luhemeja alisema.
Aliwataka wafanyakazi kujali muda wao wa Kazi kwa kutenda yale
ambayo yataondoa kero ya Maji kwa Wateja hususani kuziba mivujo ya Maji katika
maeneo mengi ya Jiji pamoja na kupambana na wizi wa Maji ili kila mwananchi
apate huduma ya Maji kihalali.
Alimalizia kwa kuwataka wafanyakazi wa DAWASCO kutekeleza kauli
ya Rais aliyoitoa mapema wakati akifungua Bunge katika sekta ya Maji pale
aliposema “LAZIMA TUWATUE AKINA MAMA NDOO KICHWANI” kwa kuhakikisha huduma ya
Maji inamfikia mwananchi na kuondokana na malalamiko ya upatikanaji huduma hiyo
kwa maeneo stahili.
No comments:
Post a Comment