Wanachama wa Chama Cha
Mapinduzi.
Ndugu zangu. Watanzania wenzangu,
Kwanza kabisa nawapongezeni kwa amani na utulivu mliouonyesha katika
mchakato wote wa Uchaguzi Mkuu ambao ulimalizika salama na hatimaye juzi
Rais wa Awamu wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John
Pombe Magufuli aliapishwa mbele ya macho yangu na ya Watanzania wengine
wengi.
Hakika tumeuthibitishia ulimwengu kwamba, sisi Watanzania ni tofauti na
wao, tunao uwezo wa kuvuka kwenye nyakati ngumu lakini bado tukabaki
wamoja tukiishi pamoja kwa upendo kama ndugu, msingi uliojengwa na wazee
wetu wa mwanzo ambao kuubomoa si kazi rahisi, kwa hili nawapongeza
Watanzania wote na ninamwomba Mungu awasaidie wenzetu wa Zanzibar waweze
kufikia muafaka utakaoleta utulivu wa taifa zima.
Baada ya kusema hayo niendeleze barua yangu niliyoianza wiki iliyopita
kwa Chama Cha Mapinduzi na Watanzania wote, hilo ndilo dhumuni la barua
hii, kuendeleza pale nilipokomea! Leo nataka kuongea baadhi ya mambo
niliyoyaona kama udhaifu mkubwa kwa Chama Cha Mapinduzi kwenye mchakato
mzima uliohitimishwa Oktoba 25, 2015 kwa wananchi kupiga kura.
Naomba
nianze na suala zima la moyo wa kujitolea katika chama, ndugu zangu hili
ni jambo la kusikitisha mno katika Chama Cha Mapinduzi, nina imani
wengi wamelishuhudia! Moyo wa kujitolea ndani ya Chama Cha Mapinduzi
umekufa kabisa, kama haujafa basi upo chumba cha huduma kwa wagonjwa
mahututi (ICU), kila kitu ndani ya chama hiki kikubwa kimekuwa POSHO,
POSHO, POSHO! Bila posho ndani ya Chama Cha Mapinduzi hakuna
kinachofanyika, moyo wa kujitolea ambao waasisi wa chama hiki
waliupandikiza wakati wa kutafuta uhuru umekufa.
Wakati katika muungano wa vyama vya upinzani, vijana walikuwa
wamehamasika, wakifanya kazi kwa kujitolea, lengo lao likiwa ni moja tu;
kuing’oa CCM madarakani, mimi nilishuhudia wanaCCM, wengine viongozi
kabisa wamekaa chini bila kufanya chochote wakisema “Tufanye nini sasa
hakuna posho?”
Kwangu mimi hii ilikuwa ni aibu, mwanaCCM anashindwa kuondoka nyumbani
kwake na kwenda kuhamasisha nyumba kwa nyumba akishawishi wapiga kura
eti hawajaletewa fedha kutoka wilayani au makao makuu, bila posho ndani
ya CCM hakuna kinachofanyika, jambo hili inabidi lishughulikiwe, moyo wa
kujitolea na uzalendo kwa chama ni lazima ufufuliwe, hii ni kazi ya
Mwenyekiti wa CCM.
Inawezakanaje vijana wa 4U Movement (marafiki wa
Lowassa) waliojiunga nchi nzima eti wafanye kazi kubwa za kututisha
kuliko jumuia za Chama Cha Mapinduzi kama ya wazazi, UWT na vijana
ambazo zina mitandao mpaka vijijini kabisa? 4U Movement wanawezaje
kufanya kazi kubwa ya kutetemesha kama jumuiya zetu hizi zina moyo wa
kujitolea? Jibu ni moja tu hapa, moyo huo umekufa sababu ya posho,
vijana wetu hawafanyi chochote mpaka wapewe posho na chama au mgombea.
Simaanishi kwamba watu wote katika jumuiya hizi hawakufanya kazi, lakini
hata wewe msomaji kama ni mwanachama wa CCM, unaelewa kabisa
ninachokizungumzia hapa ni nini na iko sababu kubwa sana ya kufufua moyo
wa uzalendo na kujitolea ndani ya chama hiki badala ya kuacha jambo
hilo lifanywe na vyama vya upinzani.
Jambo jingine ni UNAFIKI na HUJUMA
ndani ya chama, hakika tabia hizi mbili zimekiathiri sana Chama Cha
Mapinduzi kwenye uchaguzi huu. Nasema bila kupindisha, zimepunguza mno
kura za chama hiki. Kuna unafiki mno ndani ya CCM, watu sio wa kweli,
wanavaa shati la kijani mchana lakini wanavaa ngwanda la khaki usiku!
Hii ni aibu, wengine ni viongozi wa chama ngazi za wilaya, walishindwa
hata kumuombea kura mgombea urais wa chama chao kwa sababu
walishajiunganisha na kambi ya pili.
Hawa ndiyo walioendesha hujuma kukikwamisha chama kisipate ushindi
lakini ashinde mtu waliyemtaka hata kama ni wa chama pinzani, tukubali
tukatae, jambo hili lipo na ni lazima lishughulikiwe haraka iwezekanavyo
kwa usalama na ustawi wa chama, kuendelea kuwafumbia macho watu wa aina
hii itakigharimu chama kwenye uchaguzi utakaofuata.
Inawezekanaje
kiongozi wa chama akapelekewa kofia na tisheti za Chama Cha Mapinduzi
halafu akaacha kuzigawa wakati anazo stoo? Inawezekanaje akapewa posho
za mabalozi halafu akaamua kutowagawia au kukata nusu ya kiwango
alichopewa? Wakati akifayafanya haya anajua kabisa kwamba kambi ya pili
ya upinzani inagawa tisheti na kofia zake na kubandika bendera kila
mahali jimboni.
Je, hii si hujuma?
Ndugu zangu,
Niongelee mikakati, tumejitahidi sana kupambana kwenye uchaguzi huu,
naomba niwasifu watu waliokuwa kwenye kitengo cha teknohama (IT)
wamefanya kazi kubwa mno kupambana na vijana wa 4U Movement, kampeni za
safari hii ziliendeshwa kisasa na zilikuwa na nguvu kubwa sana kwenye
mitandao ya kijamii, kazi kubwa imefanywa na vijana wetu.
Lakini jambo
lililonisikitisha ni kwa nini tulikuwa mara nyingi tunakuwa wafuasi,
badala ya kuwa viongozi kwenye mikakati? Mfano Ukawa wakibandika bendera
zao nyingi mitaani ndiyo na sisi tunafuata nyuma yao, kwa nini hatukuwa
watu wa kwanza na Ukawa wakafuata nyuma? Naamini sana kwenye msemo wa
Steve Jobs usemao “Be a leader, not a follower!” daima uwe kiongozi siyo
mfuasi. Ilifika mahali ikaanza kuonekana kama timu ya Ukawa ilikuwa na
watu hatari katika mikakati kuliko sisi, jambo ambalo kwangu mimi
halikunifurahisha na ninadhani halikuwafurahisha wengi, kuna jambo la
kujifunza hapa, siku zote tuwapo katika mapambano tusiwe watu wa
kusitasita, bali tuwe watu wa kuchukua hatua za kutekeleza mawazo yetu
mara moja.
Ndugu zangu,
Sitaweza kumaliza barua hii bila kukikumbusha Chama Cha Mapinduzi juu ya
kubadilisha taswira yake kwa jamii, kisitishe mara moja tafsiri ya
kwamba ni chama cha matajiri na kurejea kwenye chama cha wakulima na
wafanyakazi ili kila Mtanzania mwenye sifa aweze kujitokeza na
atakapofanya hivyo na watu wanamkubali, apewe nafasi ya kutumikia nchi
yake, asilazimishwe tu mtu kugombea hata kama hakubaliki, sababu tu ni
mkongwe katika chama au ni waziri, hili limeigharimu CCM majimbo mengi
safari hii, kosa hili halitakiwi kuendelea kutendwa.
Katika hili ni
mpango mzima wa kutayarisha viongozi wa kesho, waliopo leo ni lazima
wataondoka, nafasi zao zitachukuliwa na akina nani? Lazima kuwe na
‘succession plan’ ya kwamba kizazi hiki kikiondoka, kitaingia hiki!
Nionavyo mimi jambo hili halifanyiki na kama linafanyika basi si kwa
kiwango kisichotarajiwa.
Lazima kuwe na “First in, first out!” yaani wa kwanza kuingia awe wa
kwanza kutoka ili kupisha wengine, ningefurahi na nitafurahi sana kuona
vijana wengi wanachukua nafasi za waliotangulia katika chama chetu ili
kuingiza mawazo ya kizazi cha sasa, badala ya chama chetu kuendelea
kutafsiriwa kama chama cha wazee kama ilivyo leo.
Yapo mengi
nitakayoyaongea kwa kirefu kwenye kitabu nitakachotoa cha kuirekebisha
CCM kwa lengo la kuijenga si kuibomoa, bado chama hiki ni chama chenye
nguvu na kinaaminiwa na watu wengi, tukikiacha kiende kama kinavyokwenda
sasa mwisho wa siku watu watakuja kupoteza imani nacho na kitakufa kama
vilivyokufa vyama vingine vilivyoleta uhuru katika nchi nyingine
Afrika, jambo hili sipendi litokee ndiyo maana nitaandika kitabu hicho.
Baada ya kusema haya, nimalizie barua yangu kwa kumpongeza Dk. John
Pombe Joseph Magufuli kuapishwa kuwa rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, nimtakie utendaji mwema wa kazi katika kuhakikisha
anazitimiza ahadi alizotoa, Watanzania wanatarajia kutoka kwake; huduma
bora za afya, upatikanaji wa maji safi na salama, elimu bora kwa kila
Mtanzania, kutokomeza ufisadi,Tanzania yenye viwanda, miundombinu bora,
amani na umoja wao kuendelea kuwepo.
Haya na mengine mengi yakifanyika, Watanzania wakafaidi utajiri ambao
Mungu amewapa, naomba nimhakikishie mheshimiwa rais ya kwamba miaka
mitano ijayo atachaguliwa tena, lakini hayo yasipofanyika, NINA MASHAKA.
Ahsanteni.
Wasalaam,
Eric Shigongo James
Wanachama wa Chama Cha
Mapinduzi.
Ndugu zangu. Watanzania wenzangu,
Kwanza kabisa nawapongezeni kwa amani na utulivu mliouonyesha katika
mchakato wote wa Uchaguzi Mkuu ambao ulimalizika salama na hatimaye juzi
Rais wa Awamu wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John
Pombe Magufuli aliapishwa mbele ya macho yangu na ya Watanzania wengine
wengi.
Hakika tumeuthibitishia ulimwengu kwamba, sisi Watanzania ni tofauti na
wao, tunao uwezo wa kuvuka kwenye nyakati ngumu lakini bado tukabaki
wamoja tukiishi pamoja kwa upendo kama ndugu, msingi uliojengwa na wazee
wetu wa mwanzo ambao kuubomoa si kazi rahisi, kwa hili nawapongeza
Watanzania wote na ninamwomba Mungu awasaidie wenzetu wa Zanzibar waweze
kufikia muafaka utakaoleta utulivu wa taifa zima.
Baada ya kusema hayo niendeleze barua yangu niliyoianza wiki iliyopita
kwa Chama Cha Mapinduzi na Watanzania wote, hilo ndilo dhumuni la barua
hii, kuendeleza pale nilipokomea! Leo nataka kuongea baadhi ya mambo
niliyoyaona kama udhaifu mkubwa kwa Chama Cha Mapinduzi kwenye mchakato
mzima uliohitimishwa Oktoba 25, 2015 kwa wananchi kupiga kura. Naomba
nianze na suala zima la moyo wa kujitolea katika chama, ndugu zangu hili
ni jambo la kusikitisha mno katika Chama Cha Mapinduzi, nina imani
wengi wamelishuhudia! Moyo wa kujitolea ndani ya Chama Cha Mapinduzi
umekufa kabisa, kama haujafa basi upo chumba cha huduma kwa wagonjwa
mahututi (ICU), kila kitu ndani ya chama hiki kikubwa kimekuwa POSHO,
POSHO, POSHO! Bila posho ndani ya Chama Cha Mapinduzi hakuna
kinachofanyika, moyo wa kujitolea ambao waasisi wa chama hiki
waliupandikiza wakati wa kutafuta uhuru umekufa.
Wakati katika muungano wa vyama vya upinzani, vijana walikuwa
wamehamasika, wakifanya kazi kwa kujitolea, lengo lao likiwa ni moja tu;
kuing’oa CCM madarakani, mimi nilishuhudia wanaCCM, wengine viongozi
kabisa wamekaa chini bila kufanya chochote wakisema “Tufanye nini sasa
hakuna posho?”
Kwangu mimi hii ilikuwa ni aibu, mwanaCCM anashindwa kuondoka nyumbani
kwake na kwenda kuhamasisha nyumba kwa nyumba akishawishi wapiga kura
eti hawajaletewa fedha kutoka wilayani au makao makuu, bila posho ndani
ya CCM hakuna kinachofanyika, jambo hili inabidi lishughulikiwe, moyo wa
kujitolea na uzalendo kwa chama ni lazima ufufuliwe, hii ni kazi ya
Mwenyekiti wa CCM. Inawezakanaje vijana wa 4U Movement (marafiki wa
Lowassa) waliojiunga nchi nzima eti wafanye kazi kubwa za kututisha
kuliko jumuia za Chama Cha Mapinduzi kama ya wazazi, UWT na vijana
ambazo zina mitandao mpaka vijijini kabisa? 4U Movement wanawezaje
kufanya kazi kubwa ya kutetemesha kama jumuiya zetu hizi zina moyo wa
kujitolea? Jibu ni moja tu hapa, moyo huo umekufa sababu ya posho,
vijana wetu hawafanyi chochote mpaka wapewe posho na chama au mgombea.
Simaanishi kwamba watu wote katika jumuiya hizi hawakufanya kazi, lakini
hata wewe msomaji kama ni mwanachama wa CCM, unaelewa kabisa
ninachokizungumzia hapa ni nini na iko sababu kubwa sana ya kufufua moyo
wa uzalendo na kujitolea ndani ya chama hiki badala ya kuacha jambo
hilo lifanywe na vyama vya upinzani. Jambo jingine ni UNAFIKI na HUJUMA
ndani ya chama, hakika tabia hizi mbili zimekiathiri sana Chama Cha
Mapinduzi kwenye uchaguzi huu. Nasema bila kupindisha, zimepunguza mno
kura za chama hiki. Kuna unafiki mno ndani ya CCM, watu sio wa kweli,
wanavaa shati la kijani mchana lakini wanavaa ngwanda la khaki usiku!
Hii ni aibu, wengine ni viongozi wa chama ngazi za wilaya, walishindwa
hata kumuombea kura mgombea urais wa chama chao kwa sababu
walishajiunganisha na kambi ya pili.
Hawa ndiyo walioendesha hujuma kukikwamisha chama kisipate ushindi
lakini ashinde mtu waliyemtaka hata kama ni wa chama pinzani, tukubali
tukatae, jambo hili lipo na ni lazima lishughulikiwe haraka iwezekanavyo
kwa usalama na ustawi wa chama, kuendelea kuwafumbia macho watu wa aina
hii itakigharimu chama kwenye uchaguzi utakaofuata. Inawezekanaje
kiongozi wa chama akapelekewa kofia na tisheti za Chama Cha Mapinduzi
halafu akaacha kuzigawa wakati anazo stoo? Inawezekanaje akapewa posho
za mabalozi halafu akaamua kutowagawia au kukata nusu ya kiwango
alichopewa? Wakati akifayafanya haya anajua kabisa kwamba kambi ya pili
ya upinzani inagawa tisheti na kofia zake na kubandika bendera kila
mahali jimboni. Je, hii si hujuma?
Ndugu zangu,
Niongelee mikakati, tumejitahidi sana kupambana kwenye uchaguzi huu,
naomba niwasifu watu waliokuwa kwenye kitengo cha teknohama (IT)
wamefanya kazi kubwa mno kupambana na vijana wa 4U Movement, kampeni za
safari hii ziliendeshwa kisasa na zilikuwa na nguvu kubwa sana kwenye
mitandao ya kijamii, kazi kubwa imefanywa na vijana wetu. Lakini jambo
lililonisikitisha ni kwa nini tulikuwa mara nyingi tunakuwa wafuasi,
badala ya kuwa viongozi kwenye mikakati? Mfano Ukawa wakibandika bendera
zao nyingi mitaani ndiyo na sisi tunafuata nyuma yao, kwa nini hatukuwa
watu wa kwanza na Ukawa wakafuata nyuma? Naamini sana kwenye msemo wa
Steve Jobs usemao “Be a leader, not a follower!” daima uwe kiongozi siyo
mfuasi. Ilifika mahali ikaanza kuonekana kama timu ya Ukawa ilikuwa na
watu hatari katika mikakati kuliko sisi, jambo ambalo kwangu mimi
halikunifurahisha na ninadhani halikuwafurahisha wengi, kuna jambo la
kujifunza hapa, siku zote tuwapo katika mapambano tusiwe watu wa
kusitasita, bali tuwe watu wa kuchukua hatua za kutekeleza mawazo yetu
mara moja.
Ndugu zangu,
Sitaweza kumaliza barua hii bila kukikumbusha Chama Cha Mapinduzi juu ya
kubadilisha taswira yake kwa jamii, kisitishe mara moja tafsiri ya
kwamba ni chama cha matajiri na kurejea kwenye chama cha wakulima na
wafanyakazi ili kila Mtanzania mwenye sifa aweze kujitokeza na
atakapofanya hivyo na watu wanamkubali, apewe nafasi ya kutumikia nchi
yake, asilazimishwe tu mtu kugombea hata kama hakubaliki, sababu tu ni
mkongwe katika chama au ni waziri, hili limeigharimu CCM majimbo mengi
safari hii, kosa hili halitakiwi kuendelea kutendwa. Katika hili ni
mpango mzima wa kutayarisha viongozi wa kesho, waliopo leo ni lazima
wataondoka, nafasi zao zitachukuliwa na akina nani? Lazima kuwe na
‘succession plan’ ya kwamba kizazi hiki kikiondoka, kitaingia hiki!
Nionavyo mimi jambo hili halifanyiki na kama linafanyika basi si kwa
kiwango kisichotarajiwa.
Lazima kuwe na “First in, first out!” yaani wa kwanza kuingia awe wa
kwanza kutoka ili kupisha wengine, ningefurahi na nitafurahi sana kuona
vijana wengi wanachukua nafasi za waliotangulia katika chama chetu ili
kuingiza mawazo ya kizazi cha sasa, badala ya chama chetu kuendelea
kutafsiriwa kama chama cha wazee kama ilivyo leo. Yapo mengi
nitakayoyaongea kwa kirefu kwenye kitabu nitakachotoa cha kuirekebisha
CCM kwa lengo la kuijenga si kuibomoa, bado chama hiki ni chama chenye
nguvu na kinaaminiwa na watu wengi, tukikiacha kiende kama kinavyokwenda
sasa mwisho wa siku watu watakuja kupoteza imani nacho na kitakufa kama
vilivyokufa vyama vingine vilivyoleta uhuru katika nchi nyingine
Afrika, jambo hili sipendi litokee ndiyo maana nitaandika kitabu hicho.
Baada ya kusema haya, nimalizie barua yangu kwa kumpongeza Dk. John
Pombe Joseph Magufuli kuapishwa kuwa rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, nimtakie utendaji mwema wa kazi katika kuhakikisha
anazitimiza ahadi alizotoa, Watanzania wanatarajia kutoka kwake; huduma
bora za afya, upatikanaji wa maji safi na salama, elimu bora kwa kila
Mtanzania, kutokomeza ufisadi,Tanzania yenye viwanda, miundombinu bora,
amani na umoja wao kuendelea kuwepo.
Haya na mengine mengi yakifanyika, Watanzania wakafaidi utajiri ambao
Mungu amewapa, naomba nimhakikishie mheshimiwa rais ya kwamba miaka
mitano ijayo atachaguliwa tena, lakini hayo yasipofanyika, NINA MASHAKA.
Ahsanteni.
Wasalaam,
Eric Shigongo James
Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu

No comments:
Post a Comment