KAMPUNI YA SIMU YA TECNO YAZINDUA SIMU MPYA YA PHANTOM 5 WENGI WAICHANGAMKIA - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA

demo-image

Post Top Ad

Tuesday, October 13, 2015

KAMPUNI YA SIMU YA TECNO YAZINDUA SIMU MPYA YA PHANTOM 5 WENGI WAICHANGAMKIA

Responsive Ads Here
1
  Meneja Mauzo wa Simu za Tecno, Freddy Kadilana akionesha simu aina ya Phanton 5 wakati wa uzinduzi wa tolea jipya la simu hizo uliofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
IMG_6375
 Wadau mbalimbli wakiwa kwenye uzinduzi huo.
IMG_6376
 Uzinduzi wa simu hiyo toleo jipya ukiendelea.
IMG_6381


IMG_6397
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
IMG_6414
  Meneja Mauzo wa Simu za Tecno, Freddy Kadilana  (kulia), akiwagawia zawadi ya simu hiyo baadhi ya waandishi waliouliza maswali mbalimbali.
IMG_6418
 Wanahabari wakipokea zawadi ya simu hiyo ya kisasa toleo jipya.
IMG_6421
Mmiliki na Mwandishi wa Habari wa Blog hii Katuma Masamba akipokea zawadi ya Tecno Phantom 5
Na Dotto Mwaibale

MAKAMPUNI yanayozalisha Simu nchini yameshauriwa kuhakikisha wanakuwa wabunifu katika kusanifu na kulizasha simu bora ili kwenda sambamba na soko la dunia.

Wito huo umetolewa na Meneja mauzo wa simu za Tecno, Fred Kadilana wakati wa uzinduzi wa tolea jipya la simu ya Phantom 5 uliofanyika Dar es Salaam juzi.

Kadilana alisema soko la bidhaa zao linakuwa kwa kasi hususan barani Afrika hivyo wanafanya jitihada kuhakikisha wanakwenda sambamba na soko la dunia.

"Soko la dunia linakuwa kwa kasi na hata bidhaa zetu pia hivyo tunajitahidi kila kukicha kwenda sambamba na ukuaji wa mahitaji ya wananchi," alisema Kadilana.

Kwa upande wake, mkurugenzi wa kampuni hiyo, Daniel Xu alisema falsafa ya kutengeneza simu bora ni kulenga mahitaji ya soko la dunia.

Alisema simu ya Phanthom 5 ni toleo linalowapa wateja usanifu wa kipekee wenye uwezo 32GB katika uhifadhi wa taarifa na pia 3 GB katika mfumo wa kusoma na kuperuzi katika simu kwa haraka zaidi.

"Simu hii ina uwezo wa 300m Ah katika betri lake hivyo kuondoa usumbufu wa kuchaji simu mara kwa mara," alisema Xu.

Xu alisema kutokana na changamoto za kidunia simu hiyo ina uwezo wa kufurahia mawasiliano katika mazingirq mbalimbali.

Aliongeza kuwa kwa kuzingatia ubora Tecno imeweza kushinda tuzo ya dunia kwa ubora na kwa sasa wanaongoza kwa mauzo kwa kipindi cha miaka mitano sasa barani Afrika.




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad