, Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni ya Zantel upande wa Zanzibar, Bwana Mohamed Musa akikabidhi hundi ya Shilingi
millioni 10 kwa Mwenyekiti wa Shule ya Msingi Mkanyageni, Bwana Ally Ngwali
Vuai shule hiyo iliyoko visiwani Pemba kwa ajili ya kukamiIisha ujenzi wa vyumba sita vya
madarasa vitakavyotumiwa na watoto zaidi ya 350
Anayeshuhudia ni Mkurugugenzi wa Mauzo Zantel Bwana Sukhwinder Bajwa pamoja na wanafunzi na
wajumbe wa kamati ya shule hiyo.
Mkuu wa Shule
ya Msingi Mkanyageni, Bwana Ramadhani Ngwali Makame, akitoa neno la utangulizi
wakati wa makabidhiano ya hundi ya shilingi milioni 10 baina ya shule hiyo na
kampuni ya Zantel kanda ya Zanzibar.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo shuleni hapo.
Kampuni ya simu za mkononi
ya Zantel leo imetoa msaada wa shilingi milioni 10 kama mchango wa kujenga madarasa
sita katika shule ya msingi ya Mkanyageni iliyopo Pemba.
Kiasi hicho cha fedha kitatumika katika kumalizia ujenzi wa
madarasa hayo sita kwa kuweka sakafu, madirisha na milango, kupaka rangi pamoja
na gharama za kazi kiujumla, msaada ambao unatarajiwa kuboresha kiwango cha elimu
katika shule hiyo.
Akikabidhi msaada huo, Mkurugenzi wa Mauzo wa kampuni ya Zantel,Bw
Sukhwinder Bajwa alisema msaada huo umelenga kuboresha mazingira ya kusomea ya
wanafunzi wa shule hiyo.
‘Kampuni ya Zantel mara zote imekuwa msitari wa mbele katika kuchangia
kujenga nchi kwa kushiriki katika kuwekeza katika shughuli za kijamii hasa
katika sekta ya elimu ambayo inaandaa mazingira na maisha bora ya viongozi wajao
katika upatikanaji wa elimu’ alisema Bwana Bajwa.
Akizungumza pia wakati wa makabidhiano hayo, Mkurungezi wa Biashara
wa Zantel upande wa Zanzibar,
Mohamed Mussa alisema Zantel imejikita zaidi katika kuhakikisha watoto wanapata
elimu bora visiwani hapa.
‘Kama kampuni inayoongoza kwa idadi kubwa ya wateja visiwani hapa
ni wajibu wetu kuhakikisha tunajitolea kwa kuwekeza katika miradi inayogusa
maisha ya wananchi kama huu wa elimu ambao unaboresha
miundombinu ili watoto wetu waweze kupata elimu bora’ alisema Mussa.
Akitoa shukurani kwa kampuni ya Zantel kwa msaada, Mwenyekiti wa
kamati ya shule, Bwana Ali Ngwali Vuai, alisema ni muhimu kuwekeza katika elimu
kwani wanafunzi wakielimishwa watakuwa sehemu muhimu ya maendeleo ya taifa letu.
‘Tunawashukuru kampuni ya Zantel kwa kutusaidia katika
juhudi zetu kuhakikisha tunaboresha mazingira ya elimu kwa watoto wetu’ alisema
Bwana Vuai.
No comments:
Post a Comment