Angalizo: Watumiaji wa mtandao wanaosema hii si akaunti yangu ni sehemu pia ya kundi lililotumia fedha kuzuia vyombo vya habari kunifikia.
— Dr Willibrord Slaa (@willibrordslaa) August 10, 2015
Nawapenda Watanzania, naiwaza kesho yake kwa aina ya vyama vya siasa vilivyopo. Tutafakari kwa makini. Mungu Ibariki Tanzania. Asanteni.
— Dr Willibrord Slaa (@willibrordslaa) August 10, 2015
Ujumbe wa CHADEMA ukiongoza na Mwenyekiti umefika nyumbani kwangu kuomba nisiongee na umma na kama nakaa pembeni nikae kimyakimya.
— Dr Willibrord Slaa (@willibrordslaa) August 10, 2015
Nimeomba ulinzi kutoka nchi na mashirika ya kimataifa. Nitakapopata ulinzi nitazungumza moja kwa moja kupitia redio na televisheni.
— Dr Willibrord Slaa (@willibrordslaa) August 10, 2015
Rushwa imetumika, demokrasia (sehemu ya jina la chama) imepuuzwa, wananchi wengi sasa ni ngumu kutuelewa tunachokiamini na kukukisimamia.
— Dr Willibrord Slaa (@willibrordslaa) August 10, 2015
Msimamo wangu ni kwamba CCM ni chafu, Lowassa ni adui wa maendeleo ya nchi hii, ameingia CHADEMA na kupewa nafasi kinyume na taratibu.
— Dr Willibrord Slaa (@willibrordslaa) August 10, 2015
Nakaa pembeni kupisha wanaodhani wana kiu ya kweli ya mabadiliko. Sitakuwa sehemu ya kampeni, sitakuwa sehemu ya maamuzi yoyote toka sasa.
— Dr Willibrord Slaa (@willibrordslaa) August 10, 2015
Sitaisaliti nafsi yangu, wala mamilioni kwa kuendelea kuwa sehemu ya uongozi na uanachama wa Chadema. Natamka kwamba NAKAA PEMBENI.
— Dr Willibrord Slaa (@willibrordslaa) August 10, 2015
Edward Lowassa ana haki kujiunga na chama chochote lakini tukumbuke kwamba ni mmoja ya uongozi mbovu ambao umeifikisha nchi hii hapa ilipo.
— Dr Willibrord Slaa (@willibrordslaa) August 10, 2015
Natamka wazi kwamba kwa nia yetu Chadema na kwa imani kubwa ya wananchi kwetu SIKUBALIANI NA MAAMUZI YA SIKU ZA HIVI KARIBUNI YA CHAMA.
— Dr Willibrord Slaa (@willibrordslaa) August 10, 2015
Wanachama wamepoteza maisha na wengine kupata vilema vya maisha Igunga, Arusha, etc. Damu yao ilikuwa sadaka kutengeneza uongozi mpya.
— Dr Willibrord Slaa (@willibrordslaa) August 10, 2015
Baada ya uchaguzi 2010 kazi imeendelea. Tumesambaza mwamko, wapo wanachama waliomwaga damu kwa imani yao kwetu kufikia nchi njema.
— Dr Willibrord Slaa (@willibrordslaa) August 10, 2015
2010 Watanzania wakaanza kubadilika, wakaonyesha njia kwa kunipa 27% ya kura za Urais katika uchaguzi uliokuwa na kasoro nyingi sana.
— Dr Willibrord Slaa (@willibrordslaa) August 10, 2015
Kwa miaka mingi nimesimama kidete kupinga ufisadi, kuwaambia Watanzania kwamba CCM haina tena uwezo wa kuwapa aina ya nchi wanayoihitaji.
— Dr Willibrord Slaa (@willibrordslaa) August 10, 2015
Nilijiunga CHADEMA nikitokea CCM takribani miaka 20 iliyopita. Nilijiunga nikiamini kwa dhati kabisa kwamba nchi yetu inahitaji mabadiliko.
— Dr Willibrord Slaa (@willibrordslaa) August 10, 2015
Nimeondolewa katika kazi zangu kama Katibu Mkuu Chadema, nimeonywa kutozungumza na vyombo vya habari na usalama wangu uko mashakani.
— Dr Willibrord Slaa (@willibrordslaa) August 10, 2015
Ndugu zangu Watanzania, hii ni akaunti yangu rasmi, bila shaka yoyote na naomba ninachoandika hapa kifikishwe kwa Watanzania popote walipo.
— Dr Willibrord Slaa (@willibrordslaa) August 10, 2015
No comments:
Post a Comment