Salaam.
Vyombo
vya habari kadhaa vimeendelea kuripoti kuhusu Katibu Mkuu wa Chama, Dk.
Slaa Kwa namna mbalimbali, Kwa leo vipo vilivyohabarisha kuwa atarejea
Ofisini leo.
Naomba
kusaidia katika hilo ili kupunguza usumbufu usiokuwa wa lazima kwa
wanahabari (ambao wanataka kujua itakuwa saa ngapi), wanachama, wapenzi,
mashabiki na wafuasi wa CHADEMA kwamba;
Kurejea kwa Dk. Slaa ofisini baada ya kumaliza likizo ya kutafakari aliyokubaliana na chama, hakutakuwa kwa siri.
Haitafanywa siri kwa sababu; kwanza hata mapumziko yake hayo hajafanywa
siri. Ufafanuzi ulitolewa Kwa uzito mkubwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa,
Freeman Mbowe.
Pili hakuwezi kuwa siri kwa sababu vyovyote vile kwa viwango vya habari,
hiyo itakuwa ni habari kubwa kwa vyombo vya habari na umma wa
Watanzania.
Tatu; haitakuwa siri Kwa sababu wanachama watapenda kushiriki jambo hilo.
Hivyo basi mara Dk. Slaa atakapomaliza mapumziko ya kutafakari na
akarejea ofisini, Kwa uzito ule ule uliotumika kusema kuwa yuko likizo
aliyokubaliana na chama, tutawataarifu Watanzania wote, vikiwemo Vyombo
vya Habari ili visiendelee kuandika tetesi ambazo zinawasababishia
usumbufu wananchi na waandishi wengine.
Makene
No comments:
Post a Comment