…………………………………………………………………………….
Na. Aron Msigwa –MAELEZO. Dar es salaam
Serikali imesema kuwa
itaendelea kuboresha miundombinu yake ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA) kote nchini ili kuwawezesha wananchi kupata huduma
mbalimbali za Serikali kwa uwazi mahali walipo kupitia mtandao.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini
Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma Bw.HAB Mkwizu wakati akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu Maendeleo ya Serikali Mtandao na malengo ya baadaye ya
uimarishaji wa matumizi ya TEHAMA katika shughuli za Serikali.
Amesema ili kuimarisha uwazi na
upatikanaji wa Takwimu huria,Serikali imeendelea kuboresha miundombinu
ya TEHAMA kwa lengo la kuwawezesha wananchi kupata huduma zinazotolewa
na Wizara na Taasisi za Serikali kupitia simu zao za mkononi mahali
walipo.
Ameeleza kuwa ili kulinda na
kuthamini mafanikio yaliyopatikana nchini Tanzania Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma, kupitia Wakala ya Serikali Mtandao(e
Government Agency) imeandaa Mkutano Mkuu wa mwaka wa wataalamu wa TEHAMA
na Watendaji Wakuu wa Serikali utakaofanyika jijini Arusha kuanzia
Agosti 17 hadi 20 mwaka huu.
Bw. Mkwizu amesema kuwa Mkutano
huo utafunguliwa na Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue chini ya
kauli mbiu isemayo Kaulimbiu ya Mkutano huo ni Uwezeshaji wa Wananchi
kupitia TEHAMA.
Amesema kuwa washiriki zaidi ya
500 kutoka taasisi mbalimbali za Serikali zinazotoa huduma kwa umma
watapata fursa ya kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano katika
kutekeleza jitihada za Serikali Mtandao nchini Tanzania, Kutafuta
ufumbuzi wa changamoto zilizopo ili kuleta maendeleo ya kiuchumi na
kijamii.
Amebainisha kuwa kupitia mkutano
huo washiriki watazungumzia namna bora ya uimarishaji wa utoaji wa
huduma kwa umma kupitia ushirikiano wa maarifa na ukuzaji wa uhusiano wa kikazi.
Aidha, wataalam wa TEHAMA wa Tanzania watapata fursa ya kujifunza kutoka. Kwa wataalam wengine wanaohusika na Serikali Mtandao kutoka nchi zinazofanya vizuri katika eneo la Serikali mtandao zikiwemo India na Singapore.
Bw.Mkwizu ameeleza kuwa wakati wa
mkutano huo mada mbalimbali zitajadiliwa zikijikita katika usimamizi wa
Serikali Mtandao nchini Tanzania, Hali ya miundombinu ya Serikali
mtandao na Utekelezaji wa Mpango wa Uendeshaji wa Serikali kwa uwazi .
Mada nyingine zitahusu uimarishaji
wa uwazi na Mfumo wa Takwimu huria nchini Tanzania na uimarishaji wa
huduma za Serikali kwa wananchi kupitia simu za mkononi na mifumo
inayotumika kutoa huduma kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment