RAIS Jakaya Kikwete ameelezea kuhuzunishwa na kifo cha mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini, Mzee Peter Kisumo ambaye alipata kuwa Mzee wa Chama cha TANU, Muasisi na mdhamini wa CCM na aliyeshikilia nafasi nyingi za uongozi ndani ya Serikali na utumishi wa umma ukiwemo uwaziri.
Katika taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu kwa vyombo vya habari jana, Rais Kikwete amesema; “Nimepokea kwa masikitiko makubwa na huzuni nyingi taarifa ya kifo cha Mzee Peter Kisumo.”
No comments:
Post a Comment