Wajumbe
walioshiriki uchaguzi wa Jumuiya ya Wandishi wa Habari Zanzibar (ZPC)
wakipiga kura kuchagua uongozi mpya katika mkutano wa Mwaka wa Jumuiya
hiyo ambao uliambatana na uchaguzi huo ambao uliofanyika ukumbi wa
Ekrotanal Mjini Unguja.
Katibu
Mpya wa Jumuiya ya Wandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) Faki Mjaka akiomba
kura kwa Wanachama (hawapo pichani)kabla ya kufanyika Uchaguzi huo.
Katibu huyo anashika nafasi ya Suzan Peter mara baada ya kushika nafasi
hiyo katika mkutano wa Mwaka wa Jumuiya hiyo uliambatana na uchaguzi
huko ukumbi wa Ekrotanal Mjini Unguja.
Na Mwashungi Tahir-Maelezo
WAANDISHI
wa habari nchini wamesisitizwa kulinda maadili ya kazi zao ikiwemo
kutumia kalamu zao vizuri hasa kipindi hiki wanapoelekea katika uchaguzi
mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Imeelezwa
kuwa ikiwa waandishi watatumia vibaya kalamu zao basi wanaweza kuvuruga
hali ya amani na utulivu na kuweka nchi katika hali ya machafuko.
Hayo
yalielezwa na Meneja Bima ya Maisha Tawi la Zanzibar Aisha Rubenic
Makorogo, wakati akifungua mkutano mkuu wa Jumuiya ya Waandishi wa
Habari uliombatana na Uchaguzi wa kuwachagua viongozi wapya uliofanyika
katika ukumbi wa Ekrotanal Mjini Unguja.
Alisema,
kazi muhimu ya wanahabari ni kuona wanaendelea kutoa elimu kwa jamii na
kutokubali kutumiwa vibaya na watu wenye maslahi binafsina badala yake
wafanye majukumu yao kwa kutenda haki kwa pande zote ili nchi iweze
kuvuka salama.
Aidha
alisema, tasnia ya habari ni tasnia muhimu katika jamii ambayo
inategemewa na kila mtu kwani inaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa wanachi
wanaoishi mijini na vijijini kupata habari zinazotokea nchini kupitia
vyombo wanavyofanyia kazi.
Meneja
huyo, aliwaomba waandishi kufanya kazi kwa ueledi wa juu ili kuona nchi
yao inaendelea kuwa na hali ya utulivu na usalama.
Hata
hivyo, aliwaomba wanachama wa ZPC kuchagua viongozi ambao wataweza
kuiimarisha na kufanya Jumuiya yao iondokane na utegegemezi wa misaada
huku wakiwa wabunifu ambao watachagua njia mbadala itakayowaletea kipato
katika jumuiya yao.
“Ili
kuweza kufanikiwa na jumuiya yenu kuimarika zaidi basi ni vyema kujenga
mshikamano na wanachama wenu na kuwa wabunifu wa kutegemea vyanzo vingi
vya kujiingizia mapato ili kuikuza jumuiya yenu,” Aliwaasa Meneja
Aisha.
Sambamba
na hayo aliwaomba wanajumuiya hao kujiunga na Bima ya maisha ambayo
inatoa fursa nyingi kwa malengo ya maisha ya baadae kwa mwanachama.
Nae
Mjumbe mstaafu wa Kamati Tendaji wa Jumuiya hiyo Suleiman Seif Omar,
akitoa shukrani kwa niaba ya wanajumuiya wenzake waliahidi kuendelea
kudumisha maadili ya kazi zao na wajibu wao katika kuitumikia jamii.
Akizungumza
kwa niaba ya Viongozi wapya Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo Abdalla
Abdul-rahman Mfaume aliwaomba wajumbe kuzidisha mashirikiano na
kuwaahidi kufanya kazi kwa moyo mmoja ili kuiletea ZPC maendeleo na
Taifa kwa ujumla.
Mkutano
huo mkuu ulimchagua Abdalla Abdul-rahman Mfaume kuwa Mwenyekiti wa
jumuiya hiyo baada ya kupata kura 40 na kumshinda mpinzani mwenzake
Suleiman Abdalla ambae amepata kura tisa,
Katibu
Mtendaji wa ZPC Faki Mjaka ambaye hakuwa na Mpinzani alipata kura 46 na
Naibu Katibu Mwinyimvua Nzukwi alipata kura 37 baada ya kumshinda
Takdir Ali aliyeata kura 13.
Makamo
Mwenyekiti wa Jumiya hiyo ni Abdalla Pandu aliyepata kura 28 na
kumshinda Rahma Suleiman aliyepata kura 23. Mshika fedha Halima Tamim
Thuwein aliyekuwa Mgombea pekee alipata kura 49 .Wajumbe sita wa kamati
tendaji ni Aziza Hassan, Ghania Mohammed, Mwashamba Haji Juma, Ishaka
Omar, Maulid Hassan Kipevu na Saleh Hassan.
No comments:
Post a Comment