Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
NYUMBU (Tanzania Automative Technology Centre) Brigedia Jenerali Anselim
akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu miradi
mbalimbali iliyotekelezwa na shirika hilo inayodhamiria kuwawezesha
wananchi kiuchumi ikiwemo utengenezaji wa matrekta madogo( power Tiller)
ambayo yanalenga kumkomboa mkulima hapa nchini kwa kuondokana na
matumizi ya jembe la makono.
Baadhi ya waandishi wa habari
wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la NYUMBU (Tanzania Automative
Technology Centre) Brigedia Jenerali Anselim.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Luteni Kanali
Juma Nkangaa Sipe akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani)
umuhimu wa kutoa habari za kuelimisha kwa jamii hasa zitakazowawezesha
kuwajengea uwezo wa kimaarifa na kuwainua kichumi kupitia elimu hiyo.
Mhandisi Mkuu Msanifu Albert
Wikedzi akiwaonesha waandishi wa Habari (Hawapo pichani) aina mbalimbali
za sanifu zinazofanyika katika shirika hilo, wakati wa ziara ya
waandishi wa habari katika kiwanda hicho Mjini kibaha.
Mhandisi Mkuu wa Karakana kutoka
Shirika la NYUMBU (Tanzania Automative Technology Centre) Ayoub Mnzava
akiwaonesha waandishi wa habari trekta ndogo (Power Tiller)
iliyotengenezwa kwa lengo la kuongeza uwezo wa wazalishaji wa mazao ya
kilimo kote nchini.
Mkuu wa Kitengo cha Usubiaji
Mhandisi Anderson Ole Zakaria akiwaeleza waandishi wa habari namna
kitengo hicho kinavyofanya kazi ili kukidhi mahitaji ya kiwanda ambapo
alisema kitengo hicho kinayeyusha hadi tani 2.5 za chuma zinazotumika
kutengeneza bidhaa mbalimbali zinazotoka katika shirika hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
NYUMBU (Tanzania Automative Technology Centre) Brigedia Jenerali Anselim
akiwaonesha waandishi wa habari moja aina ya gari la kivita
lililotengezezwa na shirika hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
NYUMBU (Tanzania Automative Technology Centre) Brigedia Jenerali Anselim
(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari
waliokuwa katika ziara hiyo,kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Luteni Kanali
Juma Nkangaa Sipe na kushoto ni mwandishi mwandamizi wa Channel Ten.
PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
…………………………………………………………………………………
Na Frank mvungi-MAELEZO
Serikali kupitia shirika la Nyumbu imebuni na kuunda trekta
ndogo (Power Tiller) kwa lengo la kuongeza uwezo wa wazalishaji wa mazao
ya kilimo kote nchini.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la NYUMBU (Tanzania
Automative Technology Centre) Brigedia Jenerali Anselim Bahati wakati
wa ziara ya waandishi wa habari iliyolenga kuona jinsi shirika hilo
linavyochangia katika kukuza uchumi wa Taifa tangu kuanzishwa kwake.
Akifafanunua kuhusu mafanikio ya shirika hilo Brigedia Jenerali
Bahati amesema limekuwa likitekeleza miradi mbalimbali kama vile
utengenezaji wa matrekta madogo( power Tiller) ambayo yanalenga
kumkomboa mkulima hapa nchini kwa kuondokana na matumizi ya jembe la
makono.
Akizungumzia moja ya sifa za matrekta hayo amesema kuwa yana
uwezo wa kulima hekta nne kwa siku na yameundwa kwa kuzingatia mahitaji
ya wananchi na dhamira ya Serikali yakumkomboa mkulima ili aweze
kuchangia kikamilifu katika kukuza uchumi.
Miradi mingine ni mradi wa gari la zimamoto (RIV) ambapo ubunifu
na uzalishaji wa magari ya zimamoto ambayo baadhi yanatumika hapa
nchini kutoa huduma ya kudhibiti majanga ya moto ambapo kupia mafanikio
ya mradi huo unaendelezwa ili kuzalisha magari yatakayotumiwa kwenye
halmashauri za Wilaya na Miji kote nchini ambapo mradi huo unategemea
ufadhili wa Serikali.
Lengo la mradi huo ni kubuni na kuzalisha magari ya zimamoto ya
gharama nafuu ili kuongeza uwezo wa halmashauri zote nchini katika
kukabiliana na majanga ya moto.
Shirika hilo pia limeendelea na kazi ya utafiti na ubunifu wa
magari ya aina mbalimbali kama vile yakubeba mizigo,kusomba maji,kubeba
mchanga na vifaa vya aina hiyo lengo likiwa ni kujenga misingi ya
kuwaletea wananchi maendeleo endelevu katika nyanya mbalimbali.
Katika utunzaji wa mazingira shirika hilo limefanikiwa kubuni
matela maalum yanayoweza kuvutwa na gari au trekta katika uondoshaji
taka kwenye halmshauri za miji na yanaweza kubeba taka tani tano kwa
mara moja hivyo kusaidia katika utunzaji wa mazingira.
Akizungumzia malengo ya shirika hilo Brigedia jenerali Bahati
amesema ni kuwa kituo cha teknolojia endelevu,chenye utawala na uongozi
bora,kuwa kituo kinachotegemewa katika utafiti na uvumbuzi wa kihandisi
nchini,kusambaza teknolojia mbalimbali nchini kwa kuzalisha kwa wingi na
kutoa huduma za uhakiki ubora kwa uhakika zaidi.
Naye Msemaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa
Luteni Kanali Juma Nkangaa Sipe alitoa wito kwa watanzania kutumia zana
zinazozalishwa na shirika hilo zikiwemo mashine za kuzalisha
matofali,pampu za kusukuma maji kwa ajili ya kilimo cha
umwagiliaji,mashine za kuchakata mazao kama korosho ili kuongeza thamani
,mashine za kuzalisha matofali na vipuri vya aina mbalimbali
vinavyozalishwa kulingana na mahitaji ya mteja.
Shirika la nyumbu (Tanzania automotive Technology Centre)
lilianzishwa Desemba 1985 lengo kuu likiwa kuwa kituo maalum cha
kufanyia utafiti na kuendeleza uvumbuzi na ubunifu wa teknolojia
mbalimbali ili kuongeza uwezo wa taifa kujiletea maendeleo endelevu
katika nyanja zote kwa kuinua uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment